Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo Agosti 7, 2026, amezindua rasmi Tume ya Rais ya Uchunguzi wa Wahusika wa Ghasia na Ukiukwaji wa Sheria katika matukio yaliyotokea wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025.
Akizungumza katika hafla iliyofanyika leo Agosti 7, 2026 Ikulu, Dar es salaam, Rais Samia amesema Tume hiyo imeundwa kuchunguza kwa kina matukio hayo, kubaini wahusika pamoja na sababu zilizosababisha ghasia na ukiukwaji wa Sheria.
Aidha, amesema Tume hiyo itatoa mapendekezo yatakayosaidia kuimarisha utawala wa Sheria, kulinda haki za Wananchi na kuzuia kujirudia kwa matukio kama hayo katika chaguzi zijazo.
“Niliunda Tume hii chini ya Jaji Shabani Lila, Makamishna Sita kutokea Nchi mbalimbali ikiwemo Uganda na Namibia, tuliamua kuwashirikisha wenzetu ili kujua ni nani wahusika, waliochochea na kutoa fedha kwa ajili ya kuhamasisha ghasia hizo,”.
“Tumepewa miezi 5 ya kukamilisha ripoti, nawasihi Watanzania kutoa ushirikiano kwa Tume, tusiisumbue,”amesema Rais Samia.






