Wachezaji wa wawili wa timu ya taifa ya Iran, Fatemeh Pasandideh na Atefeh Ramezanisadeh, wamepewa rasmi uraia wa Australia, miezi mitano baada ya kugoma kuimba wimbo wa taifa wa nchi yao.
Wawili hao waligoma kuimba wimbo wa taifa wakati wa michuano ya Kombe la Asia nchini Australia mwezi Machi 2026, hatua iliyosababisha kuitwa wasaliti na nchi yao.
Wanasoka walikaa kimya bila kuimba wimbo wa taifa wakati wa mechi dhidi ya Korea Kusini, kuonesha upinzani wao kwa utawala wa nchi yao.
Hatua hiyo, iliwafanya kuitwa wasaliti na vyombo vya habari vya Iran, hali iliyoweka maisha yao hatarini.
