Hili limejitokeza mara baada ya Lowassa kutangaza kuingia
UKAWA kupitia CDM, Kufuatia jambo hili upepo wa Dk.Slaa kupendwa na kuaminiwa
na wana CHADEMA unaelekea ukingoni kufuatia ingizo jipya, na huenda asisikike
tena katika mbio za uchaguzi mkuu akiwa mgombea wa urais wa chama hicho
kufuatia wengi kumsahau kuanzia viongozi na wanachama wa chama hicho na sasa ni
historia tu!
Dk. Slaa Kwa takribani miaka 10 ya uongozi wake amekuwa
muhimili wa CHADEMA na amekua kipenzi cha Wafuasi wa chama hicho hasa vijana
kwa ahadi zake na utumishi wake!