NADHARIA MBALIMBALI
KUHUSU CHIMBUKO LA KISWAHILI
Kiswahili ni lugha ya kiarabu.waasisi wa nadharia ni kama
vile stignd,Reusch na Knappert wanaodai kwamba Kiswahili ni mojawapo wa kati ya
lahaja ya kiarabu.vile vile wanasema kuwa utamaduni wa waswahili ni utanzu wa
waharabu
USHAIDI UNAOTOLEWA
1. Wanasema
kwamba lugha ya Kiswahili imekopa maneno mengi ya kiarabu kama
vile
a.buibui
b.daima-milele
c.fahamu-elewa
d.katibu-mwandishi
2.lugha ya
Kiswahili imefungamana na mafunzo ya dini ya kiislamu.wao hutumia majina
mengi ya kiislamu kama vile
Mohamed
Rajab
Mwanaidi
Baadhi ya maneno ya
Kiswahili yaliyokopwa kutoka kwa kiarabu yanahusiana na masaa ya waisilamu ya
kuswali.kwa mfano, alfajiri,adhuhuri,ramashari,alasiri
3.wanadai nyimbo
za taarabu ziliteuliwa kuimbwa kwa kiarabu ndipo zikaanza kuimbwa kwa mashairi
ya Kiswahili
OHLY anadai kwamba
waswahili walilazimika kutunga nakuimba mashairi ya Kiswahili yaliyoitwa
mangazi ili waepuke kufanywa watumwa na
waarabu.
4.ustaarabu wa uswahilini umebuniwa na kuimarishwa na wageni
waliotoka nchi za magharibi uarabuni,uajemi nauturuki. Ustaarabu huo ni pamoja
na mavazi kama vile buibui,mtandio,kanzu,kikoi na kofia ya kiislamu na vyakula
kama vile papuru na papai.
UPUNGUFU WA NADHARIA
HII
1.Watafiti wa lugha ya uarabuni wanasema kuwa Kiswahili si
mojawapo ya lugha ambazo zinapatikana uarabuni na hamna lahaja yoyote ya
kiswahilui.
2.kukopa maneno kutoka lugha moja hadi nyingine ni jambo la
kawaida.si Kiswahili tu kimekopa manena kutoka kwa lugha ya kiarabu. Lugha
nyingine kama kiausa,kihindu bara hindi na
kimalay huzungumzwa maleyzimekopa maneno ya kiarabu
3.kiswahili hakijakopa maneno kutoka kwa lugha ya kiarabu
bali kutoka kwa lugha nyingine. Kwa mfano hospitali, daktari na kalenda ni
kiageni, mnara,bandari,nanga klutoka lugha ya kireno mvinyo,bendera padre
parafundu
4.miji ya uswahilini kama
vile pate ,lamu na kilwa ilikuwa imestawi kabla ya waarabu kuja pwani. Madai
kwamba wageni ndio walikuja na kustawi miji ya uswahilini ni madai ya wazungu
kwa kuwa miji hii ilinyakuliwa na waarabu na wageni wengineo nah ii si sababu
tosha ya kufanya kubunuwa na wao. Haya ni madai yao tu.
Kulingana na Mbaabu kuna aina tatu za waswahili.
(1)waswahili wenye asili ya kibantu ambao walijulikana kama wangozi na waswahili wamegawanyika katika makabila
madogo madogo kwa mfano wabarawa wanaoishi Somali. Nchini Kenya makabila
hayo nikama lamu wapate,waunya,wasinyu,wamalindi,
wakilifi,wamvita,wamtang`ata,wakiingili,wanjovu na wavanga
Nchini Tanzania
kuna weamafia na watumbatu
(2)kuna waswahili waliozaliwa kutokana na ndoa kati ya
waarabu na waswahili asili.
(3)kuna waswahili waliotoka katika makabila mengine ya
waafrika. Hawa ni watu walioishi na waswahili kwa muda mrefu na kuacha mila zao
na kufuata za waswahili. Walijifanya wenyeji wa waswahili baada ya wenyeji kukutana na kusema kuwa watoe
ada iliyoitwa ada ya mji na wanati.
Baadhi yao
walikuwa watumwa na wengine waliotoka bara na kuhama.
KISWAHILI NI LUGHA YA
KIBANTU
Wafuasi wa nadharia hii ni Greenberg,
Mbaabu,Guthrie,Chimera,Chicago
na Mnyampala. Hawa wanadai kwamba Kiswahili ni asili ya kibantu kwa hivyo
inafanana na lugha nyingine kiganda,kinyamwezi na k
KISWAHILI NI LUGHA YA
MSETO
Wafuasi ni pamoja na Taylor Broomfield, steere Johnson hawa wanadai kwamba Kiswahili
ni mchanganyiko wa lugha za kiafrika na lugha za kigeni,kiarabu,kiajemi,kituni
n.k.wametoa ushaidi ufuatao ili kudhibitisha.
(1)Johnson anadai waarabu walipokuja aghalabu hawakuandamana
na bibi kutoka uarabuni kwa sababu hiyo kuliwako na uhaba wa wanawake.walianza
kufunga ndoa na wanawake wa kibantu. Watoto wao walianza kujifunza maneno ya
kiarabu kutoka kwa baba zao na maneno ya kibantu kutoka kwa mama zao kwa hivyo
vizazi vilivyofuata vikawa na lugha ya Kiswahili iliyo na mchanganyiko wa lugha
mbalimbali. Johnson anadai kwamba maneno ya kiarabu na kiajemi ambao watoto
hawa walijifunza kutoka kwa baba zao yalihusu vita,ubaharia,usafiri na vyombo
vya ufundi lakini maneno ya kibantu waliyojifunza kutoka kwa mama zao yalihusu
kilimo,ufugaji,chakula na maisha ya kila siku.
(2) Broomfield
anadai kwamba kulikuwa na haja ya waarabu kuwasiliana na watumwa wa kibantu kwa
hivyo iliwabidi kuchanganya maneno ya kibantu na ile ya kiarabu ili waweze
kuelewana wakati walipokuwa wakifanya kazi za utumwa.kutokana na mchanganyiko
huu lugha ya Kiswahili ikaibuka.
Upungufu wa nadharia
(1) Kama anvyosema
mbaabu (1978) lugha mbili katika ndoa haziwezi kuzaa nyingine kwani lugha
hazichanganyikani kama vile watu wa asili
wanavyochanganyika.
(2) Watafiti wa
Kiswahili wamedhibitisha kwamba takriban 60% maneno yote ya Kiswahili ni asili
ya kibantu, asilimi 30% ni ya asili ya kiarabu na asilimia 10% hutokana na
lugha nyingine na mbalimbali za kibantu
(3) Chimerah 1998
anasema Kiswahili sio lugha ya mseto kwa sababu sarufi haifanani na sarufi ya
kiarabu wala lugha zingine za kigeni bali inakaribiana na sarufi zingine za
kibantu
ikuyu
Ushaidi
1.ushaidi wa kihistoria
2.ushaidi wa kiisimu
(1)Ushaidi wa kihistoria
Haya ni maandishi ya kale ya Kiswahili.mashairi ya kale
yanadhihirisha kwamba lugha ya waarabu kufika pwani mashariki. Mfano wa
mashariki ya kale ni kama vile.
(a) Utenzi wa mwana
kupona
Utenzi huu una maneno mengi ya kingozi,mfano wa maneno haya
ni kama vile ng`andu-dhahabu na pulika-sikiza
(b) Utenzi wa
taambuka
Uliandikwa katika lahaja za kipate
(c) Utenzi ya
liyongo na takhmisa ya liyonga
(d) Utenzi wa
mwanakupona
(e) Habari za kiindi
HISTORIA SIMULIZI YA
MIJI YA USWAHILINI
Inapatikana katika tarihi ya lamu kiiwa na pate ambazo
zilipatikana karne nne zilizopatikana. Historia hii inazungumzia mambo kuhusu
waswahili.
(1) Katika tarihi ya
lamu tunaelezewa kwamba makundi matatu yaloyounda koo ya lamu yaliyojulikana
kwa majina ya Kiswahili ambayo ni kimanti yumbe mfumao na uungwana.
(2) Katika tarihi
yakiiwa tunaelezwa kwamba sultan wa kwanza wa kiiwa yaani iIbn Hussein
alijulikana kama lakabu naye mwanawe aliyekuwa akitawala mji wa mafia
alijulikana kama (mkoma watu) kwa vile haya ni
maneno ya Kiswahili hii inaonyesha kwamba wenyeji wa mafia walikuwa wakitumia
lugha ya Kiswahili kuwasiliana
(3) Katika tarihi ya
kipate kuna maneno mengi yaliyotumika ambayo ni pamoja na yumbe –ujumbe na
dhahabu-ng`andu
1(b) Wasafiri wa zamani
Wasafiri hawa ni kama
vile Al-masud,Al-idris,Ibn-buttata walipotembelea mwambao wa Afrika mashariki
waliona na kuandika vitabu vingi sana
kuhusu mamboa mbalimbali
Almasud-alipofika Afrika mashariki alisema kuwa aliona nchi
ya watu weusi kuanzia Sofala hadi Mogadishu
walikuwa na wafalme wao na Mungu waliyemwita Mkungulu. Alielezea kuwa chakula
cha watu nao kilikuwa ndizi na mtama. Huenda neon Mkungulu ilibadilika na kuwa
Mulungu kasha baadaye ilikuwa Mungu.
Al-indris-aliitembelea mwambao wa Afrika mnamo karne ya kumi
na akaandika kitabu kiitwacho River aliitaja miji ya Zanzibar ilikuwa Unguja. Aliandika baadhi ya
majina ya mandazi kwa mfano kisukari kikonde mkono wa tembo wa kadhalika.
Ibn batata-alizuru Afrika mashariki. Alisema kwamba
aliitembelea nchi ya Swahili alieleza kwamba watu wa Mombasa walikuwa wakinunua nafaka nchi ya
Swahili.
Msafiri mgiriki
Huyu aliandika kitabu chake cha periplus of erythrean sea. Yaani
kitabu cha maelezo kuhusu bahari hindi akiandikia mjini Alizandria miaka mia
moja iliyopita
Matatizo yanayokumba mtafiti wa Kiswahili anayetegemea
ushahidi wa kihistoria
(1) Kuna uwezekano
kuwa mambo yaliyomulikwa yalisaulika
kabla ya kuwekwa kwenye maandishi
(2) Huenda wasafiri
walionakili habari za pwani walieneza uvumi tu kama
Yule mgiriki aliyesema kuwa aliandika kitabu chake akiwa huko Alizandria
(3) Hati za kiarabu
zilizotumika kuandika miswada hazikuwa na herufi za Kiswahili hali hii
ilitatiza hali ya kutafsiri
(4) Miswada
iliyokuwa na ujumbe muhimu iliibiwa wakati wa vita mengine yakateketea kwa
kutumia moto
(5) Miswada mingine
ilifichwa na miji ya uswahilini
Maenezi ya Kiswahili
na sera ya lugha kabla ya uhuru
Kiswahili kimevuka
mipaka ya kuwa lugha ya kimataifa
Je Kiswahili kilienezwa vipi kutoka bara Kenya Uganda na
afrika ya kati Tanzania
Vyombo vitatu vilichangia maenezi ya lugha ya hii ya
Kiswahili. Vilichangia kukuza na
kusambaza Kiswahili kutoka pwani hadi bara
(a)misafara ya waarabu
(b)utawala wa wakoloni
(d)wameshenari na walowezi
Misafara ya waarabu
Misafara ya biashara ilikuwa michache kulinganishwa na Tanganyika .
Ilianza mwembe Taba,Lamu na malindi ikielekea bara kulingana na whitely misafara
ilikuwa michache kwelikweli kwa sababu zifuatazo
(1)Wamaasai walikuwa
wakali kwa vile hawakuruhusu misafara yoyote ipitie katika eneo lao la si hivyo
wangeuteka nyara
(2)Baadhi ya makabila kama
vile wakikuyu na wanandi hawakuwa na moyo wa kushirikiana na waswahili. Wawanga
tu ndio waliowaruhusu kufanya biashara na waswahili.
(3)Vita vya kuvizia vilivyopangwa na Wamazrui ili kupinga
utawala wa seyyid said viliadhiri sana
misafara hiyo
(4)Hali ya ukame iliyopatikana katika sehemu nyingi za Kenya ilikuwa pingamizi kubwa sana
kama vile ukosefu wa maji na chakula
(5)Kisiwa cha unguja kilikuwa kimetawaliwa sana
kibiashara ukilinganisha na visiwavya Kenya
kama vile lamu
(6)Tishio la wanyama pori kama vile samba hatari na nyoka
Hadhi kuu zilizofanya kieneo na kukuwa barani Afrika
(1)Hati za kiarabu
Waarabu walileta hati
zinazotumiwa katika maandishi ya lugha ya Kiswahili. Hii ni kwa sababu
hayo mambo yote yanayohifadhiwa. Ilikuwa ni kwa lugha ya maandishi ni pamoja na
fasihi ya waswahili. Kwa hivyo Kiswahili na fasihi ya waswahili. Kwa hivyo
Kiswahili kiliweza kukuwa kwa vile kingeweza kuhifadhiwa katika maandishi na
kusomwa wakati wowote.
(2)Biashara
Misafara ya wafanyibiashara ilikuwa ikitumia lugha ya
Kiswahili katika mawasiliano. Hii ilifanya lugha hii ya Kiswahili kuwabora
zaidi na kuenea zaidi. Matumizio ya Kiswahili yalijikita katika maeneo maalum.
(3)Ndoa
Waarabu waliofika pwani walifunga ndoa na wabantu. Hii
ilisababisha kizazi kipya kutokea. Hii ni kwa sababu waliyakopa maneno mengi
kutoka kwa baba na mama zao kasha lugha ya Kiswahili ikatokea.
(4)Dini ya kiislamu
Waarabu walipokuja walitaka kueneza dini yao kwa undani kabisa. Kwa hivyo iliwabidi
kuanzisha madarasa ambayo walitumia kufundishia lugha iliyokuwa ikitumiwa ni
lugha ya Kiswahili
UTAWALA WA KIKOLONI
Wajerumani walisaidia kukuza Kiswahili kwa njia zifuatazo
(1)Waliwalazimisha wafanyikazi wote wa serikali kujifunza
lugha hii ya Kiswahili. Yeyote ambaye hangeweza kukimundu Kiswahili
hangeruhusiwa kufanya kazi katika lugha ya Kiswahili hangeruhusiwa kufanya kazi
katika serikali ya ujerumani.
(2)Wafanyikazi kama vile makarani walikuwa wakihamishwa
kutoka sehemu moja hadi nyingine kwa hivyo ilikuwa ni lazima wajifunze
Kiswahili.
(3)Wajerumani wenyewe walilazimika kujifunza lugha hii.
Wajerumani walipotoka ujerumani walishauriwa wajifunze lugha hii kabla ya
kuhamia TanganyIKA
walishauriwa kujifunza kiswahili kwao hata kabla ya kuja ya Tanganyika
ambapo kiswahili UTAWALA WA KIKOLONI
KIPINDI CHA
WAJERUMANI
Watawala wa mwaka wa 1885-1916 walipokuja walikuta kwamba
kiswahili kilikuwa kimeene humu nchini kutokana na msafara wa waarabu.
Hata hivyo badala ya kutambua kiswahili
lugha ya utawala . Walitumia lugha ya kijerumani katika masomohuku
wakifunza masomo yote katika shule zote walizoanzisha lakini
shughuli hizo hazikufua dafu kwa sababu hawakuzigatia kuwa kiswahihili
ndio lugha iliyokuwa imeenea tangu wakati huo.
JINSI WAJERUMANI
WALISAIDIA KUENEZA NA KUKUZA KISWAHILI
1.Walilazimisha wafaanyikazi wote wa serikali kujivfunza
kiswashili kwa sababu pasi jua kiswahilihungeajiriwa katika serekali ya
mjerumani
2.Wajerumani walilazimika kujifunza kiswahili ili waweze kutumika katika utawala huo.
Walipotoka ujerumani kilienea Sana .
3.Watawala wa
wajerumani waliwateua watu wa jumba na diwani katika sehemu
mbalimbali za nchi kuwakilisha wanao
jifunza lugha ya Kiswahili aidha ripoti
walitoa kwa viongozi wao wajerumani ziliandikwa kwa lugha ya Kiswahili.
4.Wafanyikazi kama vile wakalimani walikuwa wakiamishwa
kutokka sehemu moja hadi nyingine na katika huamishaji Kiswahili kilitumiwa kwa
vile wafanyikazi wangepelekwa sehemu yeyote bila kujulikana wanafahamu lugha ya Kiswahili kwa hivyo wangefanya kazi kama majaji ama kwa
ofisi.
KIPINDI CHA WAINGEREZA
Waliingia baada ya vita vya kwanza ulimwenguni vilivyotokea
1914-915 waingereza walisaidia kueneza kwa njia tofauti kama :
1.walitumia Kiswahili kufundishia katika shule za misingi na kiingereza katika shule za upili na vyuo vikuu na hii ser
akueneza Kiswahili
hata kwa tabaka la chini.
2.watumishi wote wa
serekali na madhehebu yote ya
kidini walilazimika kufunza na kutumia
Kiswahili kabla ya kuanza kutumia lugha
za makabila tofauti pamoja na biashara na kilimo na uijilisti.
3.lugha ya Kiswahili ilitumiwa mahakamani katika
kushughulikia kesi za wafrika iwapo ripoti ziliandikwa kwa kiingereza na mwishowe kutafusiriwa kwa kiaswahili.
Misafara ya biashara ilikuwa michache kulingana Tanganyika
lilianza mwembeteare lamu na malindi ikipelekea bara kulingana na Whitely
misara ilikuwa michache kwa sababu ya:
1.wamasaiwalikuwa tishio kubwa kwa wafanyibiashaara kwa kutotakamisafara katika eneo lao na
mwishowe waliwadhuru wana biashara.
2.baadhi ya makabila kama
vile wakalenjin na wanandi hawakuwa na
moyo wakushirikiana na waswahili
3.vita vya kuvizia vilivyopangwa na wamazrui ili kupiga
utawala wa Seyyid Said viliadhiri sana pwani ya Mombasa na viongozi wake na
kufanya biashara kuwa hatari kufanya
na misafara mingi kutoenda bara
4.hal iya ukame
iliyopatikana katika sehemu tofauti ya
Kenya
ilikuwa pingamizi kubwa kwa wasafiri
sabau ya ukosefu wa maji na chakula
5.kisiwa cha ugunja kilikuwa kinatumiwa sana
na wafanyibiashara kilitenganishwa na visiwa vya Kenya
kama lamu na malindi.
6.tishio la wanyama pori kama vile
smba hatari na nyoka
NCHI YA KENYA
Kusudi la waingereza katika nchi ya Kenya ilikuwa kudidimiza kisu
wakitatizamaenezi kwa njia zifuatazo:
1.walitumia kisu kuendesha shughuli za utawala kama
vilekuwekeana mikataba na wenyeji
2.wai ngereza Waliwatawala wenyeji kimabavu huku wakiitumia
washauri katika kueneza Kiswahili.
3.katika elimu waingereza walisizitiza matumizi ya
kiingereza huku wakipuuza kiswahili sera hii iliimarika zaidi kwa sababu
waliofia wangetumia Kiswahili kuwaunganisha dhidi ya wakoloni kwa hivyo
waliimiza matumizi ya lugha ya kwanza katika kufunzia shuleni
WAMISHENARI NA
WALOWEZI
Walowezi hawakuathiri na kukua kwa Kiswahili nchini Tanganyika
kwa sababu walikuwa wachache. Wamishenari walikuwa wengi sana na walichangia kwa njia zifuatozo.
1.baadhi ya wamishenari walifanyia Kiswahili utafiti na
kuandika na vitabu
2.walifungua shule ambsazo zilitoa mafunzo mbalimbalibh kwa
wanafunzi wanchi hiyo
3.walianzisha vituo ambavyo kueneza kiswahnili hii ni pale
ambapo kilitumiwakatika kutoa mashauri
4.waliweza kutafsiri vitabu
vingi katika lugha ya Kiswahili mfano wa
vitabu hivi ni kama vilebibilia
6.wamishenari waliweza kuchapisha magazeti kwa lugh ya kiswahil
.magazeti hayani