MSHAURI WAKO NAMBA
MOJA
Mwanamke sahihi kwako ni yule ambaye anakushauri hasa
unapokuwa katika matatizo makubwa zaidi ya kimaisha.
Sifa hii itaonekana tangu mapema kabisa, unapokutana naye
ukiwa huna furaha, ni rahisi kukuliza kulikoni, anakuuliza si kwa sababu
anataka kuona furaha yako pekee bali pia anataka kujua kama
kuna tatizo ili aweze kutoa mchango wake wa mawazo katika tatizo lako.
Siku zote, mwanamke mwenye busara na anayekupenda, ni wazi
kwamba atapenda kujua tatizo lako na kulichukulia kama
lake, ili aweze kukushauri namna ya kutatua kwa namna moja ama nyingine.
1. KUJITOA KWA KILA
HALI
Mwanamke anayekupenda kwa dhati, atajitoa kwako kwa kila
hali. Unajua, kuna mambo ambayo si rahisi kufanyiwa na kila mtu, yapo ambayo
yanafanywa kwa watu wanaopendana tu.
Huyu atajitoa kwako, atafanya mambo muhimu ambayo si rahisi
kuyafanya kwa mtu mwingine. Atakupa vipaumbele kwenye mambo yake yote kwa
kukueleza mipango yake (hata ile ya siri) na kukufanya wa kwanza kujua
kinachoendelea katika maisha yake.
Lazima ujiulize na uangalie, je, wewe ni moja ya vipaumbele
vyake? Je, wewe unakuwa wa kwanza kujua mambo yake kabla ya rafiki zake? Je,
uzito anaochukulia kwako ukiwa na tatizo, ndiyo anaouchukua pia kwa rafiki zake
ama ndugu zake? Lazima kuwe na tofauti. Siku zote, umuhimu wako hauwezi kuwa
sawa na mfanyakazi mwenzake ofisini.
2. WIVU
Ingawa si lazima awe na wivu lakini inaelezwa kwamba wivu ni
moja ya alama ambazo unatakiwa kuziangalia wakati ukimchunguza kama anakupenda kwa dhati. Wivu ni ladha ya mapenzi. Ni
kama ndimu kwenye mchuzi au kitunguu swaumu kwenye pilau.
Wivu ni afya ya uhusiano, kwamba lazima aoneshe wasiwasi na
wewe, atilie mashaka simu yako, achunguze email yako, blog na hata ukurasa wako
wa Facebook. Hana nia mbaya, lakini anachotaka kujua, ni kama
kweli yupo peke yake au la.
3. PESA SI KILA KITU
Kama anakupenda, hawezi kuithamini sana pesa. Hiyo itakuwa kama
sehemu ya uhusiano wenu lakini si kitu anachokipa kipaumbele kwa asilimia
kubwa.
Kama anaomba sana pesa,
anazungumzia sana pesa, matatizo yake makubwa ni
ya fedha, basi ujue kwamba penzi lake
lina hati hati.
Mwenye mapenzi ya kweli, pesa ni matokeo tu, lakini si
kukufanya wewe kitegauchumi au sehemu ya kutatua matatizo yake.
4. WASIWASI NA
USALAMA WAKO
Baadhi ya wanawake wanaweza kusema mengi lakini wasiwasi kwa
ajili ya usalama wa mtu unayempenda ni muhimu sana . Hii ni moja ya njia ya kujua kama mwanamke anakupenda. Anapenda kujua uko wapi,
unafanya nini na utarudi nyumbani muda gani.
Si rahisi kufanya hivyo kwa mwanaume ambaye hana mapenzi
naye. Anafanya kwako, kwasababu anakupenda na anajali usalama wa maisha yako,
na si maisha yako pekee, bali kuna jambo kubwa na zito zaidi. Anajali usalama
wa penzi lake maana
hataki kukupoteza na kulipoteza penzi hilo .
5. ANAKUSIKILIZA
Kusikilizwa na mwanamke si tabia mpya au ya kujifunza, ni
agizo la moja kwa moja kutoka kwa Mungu mwenyewe. Kwa meneno mengine, kama mwanamke wako atakuwa hakusikilizi, mpinzani,
mkaidi, mkali, mkorofi, maana yake anapingana na maagizo ya Mungu moja kwa
moja.
Kupingana na agizo hilo ,
ambalo ni stahili yake, ni wazi kwamba hata mambo mengine ya kibinadamu ambayo
atatakiwa kujifunza yeye mwenyewe kwa nia ya kuonesha heshima kwako wewe mumewe
mtarajiwa, atashindwa.
Sipo hapa kuhubiri dini, lakini kuna mahali maandiko
yameagiza, mwanaume ampende sana
mke wake na mwanamke amheshimu/amtii mumewe.
Hapo kila kitu kipo wazi, kwahiyo katika hali ya kawaida,
kama mwanamke wako atashindwa kukutii, kukuheshimu na kukusikiliza kama kiongozi wake, basi ni dhahiri kwamba, atakuwa
tatizo katika maisha yenu ya baadaye, hasa mkiwa tayari mmeshaingia kwenye
kifungo cha ndoa.
6. ANAWAPENDA NDUGU
ZAKO
Ndugu zako ni cheni katika maisha yako. Ndiyo watu wako wa
karibu. Ndiyo wanaokusaidia/watakaokusaidia pindi utakapokuwa na matatizo.
Unapotaka kuingia kwenye uhusiano wa kimapenzi na mwanamke,
hasa kuingia katika hatua kubwa zaidi ya ndoa, unapaswa kufikiria mara mbili
juu ya hawa wanaoitwa ndugu.
Ni tatizo kubwa sana , kama mwanamke unayetarajia awe mkeo, akawa hawapendi,
anawadharau au anawachukia ndugu zako kwa sababu zake mwenyewe.
Mfano; kama mwanamke wako
hamheshimu mama yako mzazi, baba yako, kaka na dada zako ni tatizo. Inakuwa
tatizo kwa sababu hawa ni watu ambao unatakiwa kushirikiana nao katika mambo
mengi ya kijamii, hasa unapokuwa katika matatizo. Kwakuwa unawapenda ndugu
zako, pia utakuwa na mapenzi na mwanamke wako, lazima kutakuwa na mgawanyiko
maana pande hizi mbili ni muhimu kwako.
Hapa namaanisha kwamba, inawezekana kabisa ukajikuta
unaegemea aidha kwa ndugu zako zaidi au kwa mwanamke wako na hapo ndipo
mkanganyiko mkubwa wa kiuhusiano unapoweza kutokea.
Mwanamke wako akiwa na upendo na ndugu zako ni wazi kwamba
yote hayo niliyoeleza hapo juu hayatajitokeza na hivyo kuishi kwa amani.