Msanii mkongwe katika game la muziki wa kizazi kipya, an
icon, Temeke native, Juma Nature, ni moja ya wasanii waliotokea kupendwa sana
nchini Tanzania, Juma Kassim Nature a.k.a Kiroboto ameweza kumantain game na
kuendelea kuwa msanii anayependwa ingawa hajatengeneza hit siku nyingi.
“mimi ni bidhaa tayari, tena yenye ubora, toka gari aina ya
benz ilipotengenezwa zimetengenezwa gari nyingi lakini benz imeendelea kupendwa
na kuonekana ni gari bora, ila limekuwa likiboreshwa tu, hata lisipotangazwa
lakini linajulikana tayari, kwa hiyo mimi ni kama benz, nimefanya kazi nzuri
siku za nyuma you can’t take that from me, nilishatangzwa mwanzo nikafanya vizuri,
wengine lazima waje lakini nao ni bidhaa nyingine, mimi benz, wao wanaweza
kuwa, Ferrari, Cadillac, Lamborghini, Mclaren, Toyota mark x kwa hiyo kila
bidhaa na watu wake na ubora wake, kwa hiyo mimi kupendwa ni kupendwa tu”
amesema.
Pia Nature amepost kupitia instagram akiwa na Mhe. Edward
Lowassa na kuandika “Mungu yunasi mloshindwa kunitumia kikazi msinilaumu”.
maneno haya ya Nature inavyoonekana ameyaelekeza kwa wote wanaomchukulia poa
wakidhani ameshuka kimuziki na hivyo kuacha kufanya nae kazi na inavyoonekana
atakuwa amepewa kazi na Mhe. Lowassa anaweza akawa nae endapo atateuliwa
kugombea urais kupitia Chadema baada ya kuchukua fomu siku ya jana.
Kwa maana hiyo Nature atakuwa moja ya wasanii watakaofanya
kazi ya kampeni wakiwa na Mhe. Edward Lowassa katika mikoa mbalimbali nchini Tanzania .