Vitunguu ni zao la pili ambalo hutumika karibu kila siku
katika mlo wa familia za kitanzania. Afrika Mashariki, na Dunia Nzima.
Vitunguu vina chukua nafasi kubwa katika matumizi ya mboga
hasa kwa wakazi wa mijini. Vitunguu hutumika katika kutengeneza kachumbari,
kiungo cha mboga, nyama na samaki. Majani ya kitunguu hutumika kama mboga. Vitunguu pia hutumika kutengeneza supu n.k
Kilimo cha vitunguu kinaweza kufanyika kwa aina mbili
1. Green House
2. Shambani
Zao la vitunguu hustawi vizuri kwenye maeneo yasiyo na mvua
nyingi sana ,
yenye baridi kiasi wakati wa kiangazi na yasiyo na joto kali pamoja na ufukuto
wa ukungu wakati wa kukomaa vitunguu.
Zao la vitunguu hustawi vizuri kwenye udongo wenye rutuba ya
kutosha. Udongo unao ruhusu mizizi kupenya kirahisi, unao hifadhi unyevu kama vile udongo wa mfinyanzi tifutifu.
Kutayarisha shamba
Shamba litayarishwe sehemu usiyokuwa na mwinuko, sehemu ya
wazi ambayo haijalimwa
vitunguu kwa muda wa miaka 2 -3. Shamba liwe karibu na
chanzo cha maji kwa ajili ya
umwagiliaji. Matuta 1m x 3m au majaruba ya 2mx 3m.yanafaa
kwa kupanda miche. Matatu au
majaruba yanarahisisha umwagiliaji, palizi na unyunyiziaji
wa dawa.
Upandaji wa mbegu za
vitunguu
Mbegu zinaweza kupandwa kwa mstari au kwa kutawanya katika
tuta la kitalu. Katika upandaji wa mstari, mbegu hupandwa katika nafasi ya cm
10 hadi 15 kati ya mstari na mstari. Baada ya kupanda, mbegu hufunikwa kwa
udongo na baadaye kwa kuweka matandazo juu ya tuta. Mara baada ya mbegu kuota,
matandazo yaondolewe na badala yake kichanja cha nyasi kijengwe ili kuiwekea
kivuli mimea michanga. Mbegu huota baada ya siku 7 hadi 10.
Matunzo ya bustani ya
vitunguu
Umwagiliaji
Zao la vitunguu linahitaji maji ya kutosha katika kipindi
chote cha ukuaji wa mmea na hasa wakati wa kutunga tunguu. Katika kipindi
kisicho na mvua (mwezi mei hadi Agosti) Umwagiliaji ufanyike mara moja kwa wiki
kwa udongo wa mfinyanzi tifutifu na vitunguu vilivyopandwa katika vijaruba. Ili kuharakisha kukomaa kwa vitunguu unashauriwa
kupunguza kiasi cha maji ya kumwagilia taratibu kadri zao linavyo kua.
Pia ni vizuri uache kumwagilia maji mapema wiki nne hadi
sita kabla ya kuvuna. Kwani muda kamili wa kukomaa na kuvuna kwa vitunguu ni
siku 90 hadi 150 kutegemea na aina ya mbegu. Kuthibiti magugu na kupandishia
udongo Kitunguu ni zao lisilo weza kushindana na magugu. Magugu husababisha
kupungua kwa ukubwa wa kitunguu, hueneza magonjwa na husababisha kudumaa kwa
vitunguu. Katika bustani ya vitunguu, magugu yanaweza kutolewa kwa njia ya
kutifulia kwa jembe dogo, kung'olea kwa mkono na pia kwa kutumia madawa ya kuua
magugu.
Kama unaondoa magugu kwa kutifulia, epuka kutifua kwa kina
kirefu ili kutoharibu mizizi na vitunguu vyenyewe, kwani mizizi ya vitunguu ipo
juu juu sana .
Kupandishia udongo kwenye mashina ya vitunguu ni hatua muhimu ili vitunguu
visiunguzwe na jua. Hakikisha kuwa mashina ya vitunguu vyako ndani ya udongo kama sentimita 5. Pia kuna aina ya vitunguu ambavyo hutoa
au hupandisha tunguu lake
juu ya udongo wakati
vinapokua. Hivyo kupandishia udongo ili kufunika tunguu ni muhimu sana .
Hali ya hewa na maji
Hali ya hewa na maji ni vipengele muhimu sana vya kuzingatia katika uzalishaji wa
vitunguu.
Vitunguu vinastawi vizuri katika hali ya ukavu kwa kutumia
umwagiliaji. Maji mengi hasa
wakati wa masika inasababisha magonjwa mengi hasa ukungu,
vitunguu haviwezi kukomaa
vizuri, hivyo kusababisha upotevu mkubwa wa mazao. Jua na
hewa kavu ni muhimu sana
wakati
wa kukomaa na kuvuna
vitunguu.
Aina za vitunguu
Aina bora za vitunguu ni pamoja na Mang’ola red, Red creole
na Bombay Red. Hizi ni mbegu bora ambazo zinatoa mazao mengi kuanzia 40-60kgs
kwa hekta. ikiwa kilimo bora kitazingatiwa. Mkulima anaweza kuchagua mbegu kwa
kuzingatia:-
Mahitaji ya soko (vitunguu vyekundu hupendwa zaidi)
Msimu wa kupanda
Uwezo wa kuzaa mazao mengi
Uwezo wa vitunguu kuhifadhiwa kwa muda mrefu.
Mbegu bora
Ubora wa mbegu ni muhimu sana , kwani ndiyo chanzo cha mazao bora.
Mbegu bora inatoa miche yenye afya na kuzaa mazao mengi na bora. Mbegu za
vitunguu inapoteza uoto wake upesi baada ya kuvunwa (mwaka1). Mbegu nzuri zina
sifa zifuatazo:-
Uotaji zaidi ya 80%
Mbegu safi
zisiyo na mchanganyhiko
Zimefungwa vizuri kwenye vyombo visivyopitisha hewa na
unyevu.
Hivyo mkulima
anaponunua mbegu za vitunguu azingatie yafuatayo:
Chanzo cha mbegu
Tarehe ya uzalishaji
Tarehe ya kuisha muda wa
Kifungashio cha
mbegu.
Inashauriwa mkulima asipande mbegu zenye umri zaidi ya mwaka
mmoja
Mbegu bora za
vitunguu zinauzwa na makampuni binafsi kama :
ALPHA Seed Co,
Popvriend,
· Rotian Seed,
· Kibo Seed,
· East African Seed
Company nk.
Wasambazaji wa mbegu
ni pamoja na maduka ya TFA, na maduka ya pembejeo za kilimo katika maduka
mbalimbali.
Nikutakie siku njema na kilimo bora, katika makala ijayo
tutaangalia magonjwa yanashambulia vitunguu na jinsi ya kuweza kuyazuia.