Oparesheni hiyo ilishirikisha mamia ya wafanyikazi waliokuwa
wakiandaa vipuri vya simu vilivyotumika kama
simu mpya aina ya iphone tayari kuuzwa nje,huku simu hizo bandia zikizalisha
kitita cha dola miloni 19.
Kampuni hiyo iligunduliwa tarehe 14 mwezi Mei lakini
ikabainika katika mitandao ya kijamii na ofisi ya usalama ya umma Beijing siku ya jummapili.
Oparesheni hiyo ilianzishwa mwezi wa januari.
Uchunguzi huo uliongozwa na kundi la mke na mumewe kaskazini
mwa mji mkuu wa Uchina, kulingana na mamlaka ya Beijing , Walisema kuwa walidokezewa na
mamlaka ya Marekani ambayo ilinasa simu hizo bandia .
Ripoti hiyo inajiri wakati kuna msako wa bidhaa bandia
unaotekelezwa na Uchina huku mamlaka hiyo ikiyashinikza makampuni kuweka nembo
za ubora wa biadha, Uchina pia imekubali kufanya kazi na mamlaka ya Marekani
kupunguza kuwepo kwa bidhaa bandia zinazotoka nchi hizo mbili.