Nguli wa soka Duniani ,Diego Maradona amemtuhumu mke wake wa
zamani Claudia Villafañe kwamba kumuibia kiasi cha fedha zipatazo dola milioni
tisa, katika akaunti yake ya benki.
Akizungumza katika matangazo ya moja kwa moja ya
Luninga,Maradonna amesema Villafañe ambaye alikuwa mpenzi wake wa zamani ni
mwizi. Hata hivyo Villafañe amepinga vikali madai na kudai kuwa yeye si mwizi
na hakuiba fedha hizo.
Wapenzi hao ambao walikutana katika mji uliokithiri kwa
umasikini huko Buenos Aires
kabla ya Maradonna kuwa maarufu na kuwa miongoni mwa wachezaji mahiri duniani
katika historia ya soka,waliachana kimapenzi kutokana na kutofautiana.
Watoto wao wawili Dalma and Giannina,wamekaririwa kwenye
mtandao wa twitter wakimtetea mama yao wazi wazi
na kwamba hahusiki na upotevu huo wa fedha za baba yao .