Akipiga stori na gazeti hili, Wastara ambaye alishika nafasi
ya pili katika kinyang’anyiro hicho, alisema amefurahi kwa nafasi hiyo kwani
amethubutu na hakuitegemea, hivyo anajipanga kuwa karibu na walengwa wake ambao
ni walemavu ili kujua matatizo na malalamiko yao .
“Ukweli nimejitahidi sana maana nimeshindana na mtu aliyekaa
madarakani kwa miaka 20 na ni mara yangu ya kwanza kugombea ubunge,
nimethubutu, nimepata kura 254 siyo mchezo japo anayetakiwa ni mmoja lakini
jina langu litaenda kujadiliwa na nitafikiriwa,” alisema Wastara ambaye
alibwagwa na Magreth Mkanga.