Mwigulu Ahojiwa Masaa Matatu na TAKUKURU..Kisa Hichi Hapa

Wanajamvi, kale kamchezo ka Mwigulu kujiona yupo juu ya sheria na kutoa rushwa kila kona ya Iramba imemtokea puani baada ya kukamatwa na kuhojiwa na Takukuru kwa muda wa zaidi ya masaa matatu.

Wagombea wenzake walijitoa katika kinyang'anyiro tangu tarehe 25 kwa madai ya kufanyiwa rafu hizo na kutoa malalamiko yao huku wakisubiri suala hilo kushughulikiwa ndipo warejee kwenye kampeni.

Ofisi ya Takukuru mkoani Singida imemuhoji kwa masaa kadhaa naibu waziri wa fedha na aliye kuwa mbunge wa Iramba Magharibi Mheshimiwa Mwigulu Nchemba, kwa tuhuma za kukiuka sheria ya garama ya uchaguzi na sheria ya kuzui na kupambana na rushwa.

Akiongea na waandishi wa habari mkuu wa Takukuru mkoani Singida Bwana Joshua Msuya amesema Mheshimiwa Mwigulu Nchemba amekiuka sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa namba 11/2007 katika zoezi linalo ndelea la kura za maoni ndini ya vyama vya siasa.

Katika hatua nyingine Bwana Msuya amewatahadharisha wagombea wote wa ngaza mbalimbali watakae jihushisha na kutoa rushwa iwe ya fedha au vitu,vifaa vya michezo, madawati watakuwa wamekiuka sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa namba 11/2007 na sheria ya uchaguzi cap.343 r.e 2002 na pia sheria ya garama za uchaguzi namba 6/2010.

Katika jimbo la Singida kaskazini wa tia nia saba ambao wanagombea ubunge kwa tiketi ya CCM, wametishia kujitoa katika kinyanganyiri hicho kufuatia msimamizi wa uchaguzi kumwachia mgombea mwenzao ambaye ndiye mbunge wa jimbo hilo kuto kufuata masharati ya sheria za uchaguzi jambo ambalo limekuwa kero hadi kutumia vijana wa shule kuonyesha vipeperushi vyake wakati wa mkutano wa kujinadi.

ITV haikuishi hapa ilifanya juhudi za kumwona kaimu katibu wa CCM mkoa wa Singida ambaye ndiye msimamizi mkuu wa mkoa Bwana Aluu Segamba, amekiri kuwepo kwa matatizo hayo na kuchukuwa jukumu la kumbadilisha msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo na kumweka mwingine.


Baadhi ya majimbo ya uchaguzi yenye wabunge ambao wameamua kutia nia ya kugombea tena wamekuwa wakioneka wao ni chanzo kimoja wapo kikubwa cha kuvunja mashariti ya uchaguzi na kuwasababishia wenzao kuwa na malalamiko mengi,hadi kufikia hatua ya kuiomba serekali kupeleka maafisa wa takukuru na polisi kwenye mikutano ya kujinadi kugombea ubunge.