Hatimaye Mheshimiwa Ndugai amechimbia kaburi la kisiasa
baada ya kumshambulia Mgombea mwenzake aitwae Dr Joseph Elieza Chilongani kwa
gongo katika mkutano wa kuomba kupigiwa kura za maoni CCM
Hayo yametokea jana mnamo saa saa 10 jioni katika kitongoji
cha ugogoni mjini Kongwa.
Katika kile kinachoonekana ni kuishiwa sera na kutumia ubabe
na ukorofi ili kutetea nafasi yake ya kugombea ubunge wa Jimbo la Kongwa,
Mheshimiwa Naibu Spika wa Bunge La Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mbunge wa
Jimbo la Kongwa alipiga kwa gongo ambalo amekuwa akitembea nalo huku wasimamizi
wa uchaguzi wakifumbua macho kitendo cha mgombea kutembea na silaha hiyo kwenye
kampeni.
Inadaiwa na mtu aliyefuatilia kwa karibu tukio hilo mkutanoni kuwa Kuna
mgombea mmojawapo (mkazi wa Kongwa aitwaye ngatunga) Alisimama kuuza sera zake
na kudai kuwa Kongwa kuna madini jimbo halijafaidika na chochote kutoka kwa
wachimbaji wa madini... Mara moja Ndugai alimtishia kuwa anyamaze la sivyo
angemuonesha kazi kwa kile anachodai kuwa ni kuongea upuuzi..
Wakati wagombea hao wakiendelea kujibizana suala hilo ndipo ghafla
mheshimiwa alipomuona Mmojawapo wa wagombea aitwaye Dr Joseph Chilongani
ameshika simu na kutahamaki kuwa alikuwa akimrekodi kwa kuvunja taratibu.
Ndipo Job Ndugai alipoamka na kumwambia "Tena wewe
nilikuwa nakutafuta siku nyingi sana ,
unanirekodi na makamera yako na leo utanitambua mimi ni nani."
Mara Ndugai akakusanya nguvu na kumpiga Dr Chilongani kwa
fimbo hiyo. aidha hata baada ya kuanguka chini Ndugai alimfuata na kumrukia
kumkanyaga tumboni akiwa na hasira na nia ovu ya kutaka kumdhuru zaidi..
Baadae wananchi walipata hasira na kutaka kumshughukilia kwa
kichapo Mbunge huyo na ndipo alipopanda haraka gari lake haraka
na kukimbi Eneo la Tukio..Inasadikiwa yule mgombea mwingine alijaribu
kumnyanyua Dr. Pale chini, jambo ambalo baadhi ya wananchi walilichukulia ni kama kutaka kumdhuru zaidi hivyo walianza kumpa kichapo
huyo mgombea mwengine kiasi hadi watu wengine walipoamulia.. Baada ya tukio hilo ovu mkutano
ulivurugika.
Ndugu zake Dr. Chilongani kwa kusaidiana na watu walimbeba
akiwa amezimia na kumkimbiz hospital baada y kupata PF 3 toka polisi.
Hadi reporter anaondoka hospitalini Dr alikuwa bado
hajazinduka na madaktari walikuwa wanaendelea na harakati za kuokoa maisha ya
mgombea huyo.
Shuhuda mmoja wa tukio anasema kuwa tukio hilo lilirekodiwa na pengine ushahidi huo
utatumika katika kumuengua Ndugai katika kinyanganyiro cha ugombea ubunge kwa
ticket ya CCM hasa baada ya watia wengine kuweka pingamizi mara mbili lakini
bado uongozi wa chama ulikuwa unafumbia macho.
Baadhi ya wanachama wa CCM walidai kuwa kama
haki itatendeka Ndugai atakuwa amejichimbia kaburi la kisiasa na kushuhudia
KIAMA CHAKE RASMI KATIKA SIASA ZA JIMBO LA KONGWA..