Wiki chache
zilizopita tarehe 6
JULY 2015 mahakama
ya Kisutu ilitoa
hukumu katika kesi maarufu
na ya muda
mrefu iliyokuwa ikiwakabili
mawaziri wa zamani
wawili na katibu
mkuu mmoja. Blog
hii iliripoti kwa
ufupi sana kuhusu
matokeo ya kesi
hiyo na kuahidi
kutoa ufafanuzi wa
kitaalam hapo baadae
kupitia wanasheria wake. Kwakuwa
MICHUZI blog imekuwa
mstari wa mbele
kueleza masuala ya
msingi ya kijamii yakiwemo yale
ya kisheria ambayo
hayapatikani mitandao mingine ya
kijamii imeona ni
muhimu kuufafanulia umma nini
kilitokea katika kesi hii
mwanzo hadi mwisho. Tunaanza
hivi.
1.NANI WALIKUWA
MAHAKIMU KATIKA KESI HIYO.
Walikuwa
mahakimu watatu. Wa kwanza
ni S,M Rumanyika hakimu mkazi
mwandamizi ( PRM), Wa pili ni S.
Kinemela hakimu mkazi mwandamizi
Na ndugu Utamwa kama
hakimu mkazi mwandamizi ( PRM) japo kwasasa
ni jaji wa
mahakama kuu. Kesi husika
ilikuwa kesi Namba
1200 ya mwaka 2008. Mahakama iliyosikiliza
kesi hiyo na
kuitolea maamuzi ni mahakama ya
hakimu mkazi ( RM),kisutu.
2. NANI WALIKUWA
WASHITAKIWA .
Mshitakiwa wa kwanza
alikuwa ndugu Basil
Mramba Pesambili aliyeshitakiwa kwa
nafasi yake ya
uwaziri wa fedha
na uchumi wakati
makosa yanatendeka. Wa pili
alikuwa ndugu Daniel Aggrey Ndhira
Yona aliyeshitakiwa kwa
nafasi yake ya
uwaziri wa nishati
na madini wakati
makosa yalipotendeka. Na wa tatu
alikuwa ndugu Grey Shwaibu
Mngonja aliyeshitaiwa kwa
nafasi yake ya
ukatibu mkuu wa
wizara ya fedha
na uchumi wakati
makosa yakitendeka.
3. NI MAKOSA
GANI WALISHITAKIWA NAYO.
( 1 ) Kosa la Kwanza,
ni kuwa ndugu
Mramba akiwa waziri
wa uchumi na
fedha na ndugu Yona
akiwa waziri wa
nishati na madini
wote kwa pamoja kati
ya August 2002 na
June 2004 bila
kufuata utaratibu walitoa
zabuni na kuingia
mkataba na kampuni
ya MS ALEX STUWART kufanya kazi
ya ukaguzi wa madini
yanayozalishwa kinyume na
sheria ya manunuzi
ya umma Sura ya 410
ya 2002, na
kinyume na sheria
ya madini Sura ya
123 ya 2002
na kuathiri maslahi
ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania.
( 2 ) Kosa la pili,
May 2005 kwa nyadhifa zao
hizohizo bila kufuata
utaratibu waliiongezea mkataba wa
ukaguzi wa madini
kampuni hiyohiyo ya Alex
kwa miaka miwili zaidi
kuanzia tarehe 14 JAune 2005
hadi tarehe 23 June 2007. Na kuwa
nyongeza ya muda
ilifanywa na watuhumiwa
kwa kuizunguka kamati
malum ya serikali ( Government Negotiating
Team GNT) iliyokuwa imeteuliwa
kusimamia mchakato huo.
( 3 ) Kosa la tatu, ni
kuwa kati ya March
na May 2005 mawaziri
hao wawili kwa nia
mbaya walizuia taratibu
halali za kimkataba
zilizopendekezwa na mwanasheria
mkuu pamoja kamati
ya serikali ( Government
Negotiating Team GNT) iliyokuwa
imeteuliwa kwa kazi
hiyo.
(4 ) Kosa la nne,
December 2003 mshitakiwa
wa kwanza Mramba na
watatu Mgonja bila kufuata
utaratibu walitoa tangazo la
serikali GN No. 423/2003
wakitoa msamaha wa
kodi kwa kampuni
ya Alex Stuwart na baadae
tangazo namba 424/2003
yote kwa kuipendelea
kampuni hiyo isilipe kodi.
( 5 ) Kosa la tano,
ni kuwa Mramba na Mngonja
bila kufuata utaratibu
tarehe 15/ 10/ 2004 walitoa
tangazo jingine la
msamaha wa kodi
kwa kampuni hiyohiyo
GN No. 497/2004 na GN NO. 498 /2004
( 6 ) Kosa la la
sita, ni kuwa
watuhumiwa wote watatu
kati ya mwaka
2003 na 2007 kwa nafasi
zao waliisababishia serikali
hasara ya Tshs 11, 752, 350, 148/= ikiwa kama
kodi( income & withholding tax) .
Kwa ujumla
makosa yalikuwa kumi
na moja lakini
kwakuwa mengi yanafanana ukiyaunganisha unapata
hayo sita niliyoeleza.
4. NI MAWAKILI
GANI WALISIMAMIA KESI
HIYO.
Upande wa mashtaka kulikuwa na
Wakili wa serikali
Mwandamizi Osward Tibabyekomya
akisaidiwa na wengine
wakiwemo wa Taasisi
ya kuzuia na
kupambana na rushwa.
Upande wa wa
utetezi Mramba alitetewa
na mawakili wawili H.H.H Nyange na P. Swai. Ndugu Yona
alitetewa na na
mawakili wawili pia C. Tenga
na E. Msuya wakati Mngonja
naye akitetewa na
mawakili wawili Profesa
Shaidi na Malimi.
5. NANI WALIKUWA MASHAHIDI UPANDE
WA MASHITAKA NA
WALISEMA NINI ?.
Mashahidi upande wa
mashitaka ni mashahidi
ambao hutoa ushahidi ili
kumtia hatiani/kumfunga mtuhumiwa.
( A ) SHAHIDI WA
KWANZA.Huyu ni ndugu
Nyelo Martin Hiza. Kipindi
makosa yanatendeka alikuwa
mkuu wa idara ya
sheria na baadae
kamishna wa madini
katika wizara ya nishati
na madini. Anasema yeye
alikuwa mmoja wa wana timu
iliyokuwa ikishughulikia mchakato
wa kupatikana kwa kampuni
ya ukaguzi wa
madini. Anasema kwamba kampuni
iliyopatikana ilikuwa Alex Stuwart. Anasema pamoja na
kupatikana kampuni hiyo lakini ilikuwa haina
mtaji na yeye haraka
aliripoti jambo hilo
kwa mtuhumiwa wa
pili Daniel Yona. Anasema pia
viwango vya tozo
za kampuni hiyo
vilikuwa vikubwa na walitoa
mapendekezo kuhusu hayo yote
ambapo hata hivyo mapendekezo yao hayakuzingatiwa na watuhumiwa.
Pia anasema
alipewa kazi ya
kutafiti utendaji wa
kampuni hiyo ambapo
anasema aligundua utendaji wake
ulikuwa chini ya 15%
na alitoa taarifa
hiyo ambayo hata
hivyo nayo ilipuuzwa na
watuhumiwa. Anasema baadae kampuni
hiyo ilielemewa na kushindwa kabisa
kutekeleza majukumu yake ambapo
walitoa mapendekezo kuachana
nayo na kutafuta
mzabuni mwingine. Hata
mapendekezo hayo nayo hayakuzingatiwa ambapo
mawaziri hao waliamuru
mchakato kuendelea.
( B ) SHAHIDI WA
PILI. Huyu ni Betha. H. Soka.Yeye alikuwa
mkurugenzi wa kitengo
cha manunuzi ya
umma(PPRA) na mmoja wa
wanatimu iliyokuwa ikiratibu
mchakato huu wa kampuni ya kukagua
madini. Anasema aliitwa
benki kuu kujadili mchakato wa
mkataba wa kampuni ya ukaguzi
wa madini. Anasema jambo la
kushangaza masharti ya
mkataba yalikuwa sio
ya kujadili ila yalikuwa tayari yameandaliwa na sharti
mojawapo ndani yake likiwa msamaha wa
kodi. Anasema alipofika katika
kikao hicho wakurugenzi
wa kampuni ya
Alex walikuwa tayari
nao wapo pale. Hivyo yeye alipewa
tu mkataba kupitia na
hivyo hakuchangia katika kuuandaa.
Anasema kwa
kuupitia alishauri kutokuwepo
kwa msamaha wa kodi. Anasema alishauri
hivyo kwa kutambua kuwa
watuhumiwa hawakuwa wanasheria
na hivyo walistahili kushauriwa kuhusu hilo.
Hata hivyo pamoja
na ushauri huo
wa kitaalam bado
kifungu cha msamaha
wa kodi kiliendelea kubaki. Anasema TRA nao
walishauri kuwa hakuna msamaha
wa kodi. Anasema baadae
alikuja kugundua kuwa
ushauri wao uliombwa
wakati ambapo mtuhumiwa
wa Mramba na
Yona walikuwa tayari
wameingia mkataba na
kampuni ya Alex. Waliingia
mkataba kwanza halafu
ndio wakaomba ushauri, kitu ambacho kiliufanya ushauri
wao kuwa sawa na
bure.
( C ) SHAHIDI WA TATU. Huyu
ni Aggrey Temba. Yeye alikuwa
mwanasheria mkuu wa
TRA. Anasema aliombwa ushauri
kuhusu msamaha wa
kodi kwa Kampuni
ya Alex. Anasema
walishauri hakuna msamaha
wa kodi na hata
kamishna mkuu wa
TRA alishauri hivyo. Anasema wizara ya
fedha kupitia Mramba
ilikubali kuondoa kipengele
cha msamaha wa kodi ambacho
baadae kumbe kilirudishwa
kinyemela na Mramba
pamoja na wenzake. Anasema baadae
hata wao TRA
waligundua kitu kingine kuwa hata
ushauri walioombwa ilikuwa
ni baada
ya watuhumiwa kuwa
tayari wamekamilisha mkataba
hivyo ushauri
wao ilikuwa bure.
( D ) SHAHIDI WA NNE. Huyu
ni George A.C Ntigiti. Yeye alikuwa
mhasibu mkuu wa serikali .
Anasema alipata taarifa
kutoka TRA kuhusu
jambo hilo naye
mara moja akawashauri
watuhumiwa kuwa hakuna
msamaha wa kodi
kwa kampuni hiyo.
( E ) SHAHIDI WA TANO. Huyu
ni Grey Lazaurus Mwakalukwa. Yeye ni mkurugenzi
mkuu wa STAMICO. Anasema yeye
alishauri kuhusu tozo
za kampuni hiyo. Anasema
alihoji watuhumiwa kuhusu
kuikubali kampuni hiyo iendelee kuitoza
serikali tozo kubwa
kuliko inavyofanyika sehemu yeyote
duniani. Alishauri kuwa ili kujiridhisha wafanye
utafiti katika nchi
nyingine ambapo walifanya
utafiti nchi za Australia, Peru, Chile na
South Africa na kugundua
kuwa tozo ziko
chini kuliko kampuni
hiyo ilivyokuwa ikiitoza
serikali ya Tanzania.
Kutokana na hilo waliwashauri
watuhumiwa kuachana na kampuni
hiyo na kutangaza tenda
upya jambo ambalo halikufanyika.
( F ) SHAHIDI WA SITA. Huyu ni Kambona
kutoka mamlaka ya
kuzuia na kupambana
na rushwa(TAKUKURU). Anasema
kuwa katika upelelezi
wake aligundua kuwa
watuhumiwa walishauriwa karibia
na kila idara kuwa
kusiwepo na msamaha wa kodi kwa
kampuni ya Alex. Anasema
hata hivyo katika
upelelezi wake aligundua
kuwa mmoja wa wanahisa
wa kampuni ya Alex
aitwaye GEORGE alikuwa
MTOTO WA MRAMBA.
Mashahidi jumla walikuwa
13 lakini hao
niliotaja ndio walikuwa
wa msingi zaidi. Pamoja na
hayo hata hao
ambao sikutoa maelezo yao nao walitoa ushahidi
unaofanana na wa
hawa ambapo walieleza kutokuwepo
msanaha wa kodi, uwezo
mdogo wa kampuni hiyo,
kukiukwa kwa taratibu katika
kuipata kampuni hiyo
na kuiongezea mkataba
mpya kinyemela.
Zingatia, mashahidi
waliyaeleza haya kwa
kutoa nyaraka kusapoti kila wanachosema.
6. ALIVYOJITETEA MRAMBA.
Kwa tuhuma hizo
na ushahidi huo mramba
alijitetea kwa kusema kuwa,
kwanza yeye kama waziri
wa fedha na uchumi sheria imemruhusu kutoa msamaha wa
kodi na hivyo alitumia
sheria hiyo kutoa msamaha huo.
Pili alisema alipata maelekezo
kutoka ikulu kwa rais
Mkapa yakimtaka kuendelea
na mchakato mara moja
na hivyo alikuwa akitekeleza maagizo ya mkubwa
wake. Tatu pesa
ya awali iliyolipwa kwa
kampuni hiyo kutoka benki
kuu kiasi cha dola
milioni moja anadai
hakuhusika kuishinikiza
benki kuu kulipa fedha
hiyo kwa kuwa
hana uwezo wa kuishinikiza benki ambayo wakuu
wake hawawajibiki kwake isipokuwa
kwa rais .
Pia anakubali kuomba ushauri
TRA kuhusu msamaha wa
kodi lakini anasema kuwa
hakuwahi kupokea ushauri wao
kama wao wanavyodai.
7. ALIVYOJITETEA DANIEL
YONA.
Naye kubwa zaidi kwake
ni kuwa rais
Mkapa aliwaambia kutekekeleza
mchakato huo kwa
haraka na ndio
maana waliamua kuendelea
nao haraka. Utetezi wake
ni sawa na wa
Mramba katika nukta
nyingi kwakuwa wote
walishitakiwa kwa makosa
yanayofanana.
8. ALIVYOJITETEA GRAY
MNGONJA.
Anasema kuwa kipindi
akiwa katibu mkuu
kulikuwa na makatibu wakuu
wa tatu kwa wakati mmoja
ambao walifanya kazi
bila mipaka maalum
ya majukumu. Anasema
ushiriki wake katika
kuandaa matangazo ya serikali
yaliyotoa msamaha wa
kodi alikuwa akitekeleza
maagizo ya bosi
wake Mramba. Anasema yeye
aliagizwa kuandaa na akafanya
hivyo. Na kusingekuwa na
namna ya kutofanya
hivyo.
Zingatia, hawa nao
waliyaeleza haya kwa
kutoa nyaraka kusapoti kila wanachosema.
9. MAWASILISHO YA
MWISHO YA MAWAKILI
WA WA AKINA MRAMBA.
Wakati wakifunga utetezi
mawakili wa washitakiwa
walitumia kesi ya
JONAS NKIZE v R (1992) TLR 213
inayosema kuwa lolote
ambalo limefanyika au
kutofanyika(commission & omission) lazima liwe
limeelezwa katika sheria.
Wakasema kutokana na
hilo sheria inasema kuwa kodi
ambayo haijalipwa huwa
haiitwi hasara na
hivyo ni makosa
na sio kweli kusema
watuhumiwa waliingizia serikali
hasara.Wakasisitiza kuwa kodi
iliyosamehewa na watuhumiwa
ilikuwa haijaingia mikononi
mwa serikali na
hivyo sio hasara na
ni makosa kusema watuhumiwa wameiingiza
serikali hasara.
Pili kuhusu matumizi mabaya ya ofisi mawakili
wakatunmia kesi ya PETER
PROTASE v R (1970) HCD 169
ambayo inasema kuwa
matumizi mabaya ya
ofisi ni tendo
ambapo mtumishi wa
umma kwa nia
mbaya, bila kufuata
sheria na kwa
malengo binafsi anakiuka
haki za wengine na
kusababisha hasara. Kwahiyo wakasema
kuwa kwa tafsiri
hiyo hakukuwa na
ushahidi kuwa watuhumiwa walikuwa na
nia mbaya, na
wala ushahidi kuonesha maslahi
binafsi na wala
hakukuwa na hasara yoyote. Kwa
tafsiri hii wakasema
kuwa matumizi mabaya
ya ofisi hayakuwepo na
wakaiomba mahakama isilikubali
kosa hilo.
10. MRAMBA NA
YONA WATIWA HATIANI.
Kwakuwa
watuhumiwa walijitetea na kubwa
zaidi wakisema wao
hawakuwa na mamlaka katika
kusamehe kodi bali
walipokea maelekezo kutoka
kwa rais Mkapa
mahakama ilitakiwa ilijibu
hilo kwanza.
Mahakama ilisema hivi, watuhumiwa wamekiri
kuwa wao ndio
walioteua kamati ya
kutafuta mzabuni, na kamati
hiyo iliwajibika na
kuripoti kwao kila
hatua. Kwa nukta hiyo
mahakama ikakataa kuwa
si kweli kuwa
hawakuwa na mamlaka
katika mchakato kama
walivyodai. Mahakama ikasema
zaidi kuwa ni
kweli rais Mkapa
aliruhusu kuendelea kwa
mchakato haraka lakini
alifanya hivyo baada
ya watuhumiwa kuwa
wamemshauri kuhusu jambo
hilo kama washauri
wake. Na mbaya zaidi
ushahidi unaonesha kuwa
taarifa aliyopelekewa mkapa na
watuhumiwa kuhusu kampuni
hiyo haikugusia lolote
kuhusu msamaha wa
kodi wala tozo
za juu zilizokuwa
zikitozwa na kampuni
hiyo.
Hivyo kutokuwepo kwa
taarifa hizo kulimfanya
mkapa kuamini kuwa
ni kampuni safi na
hivyo kutoa maagizo
ya kuendelea haraka
na mchakato.
Lakini zaidi mahakama
inasema kuwa ushahidi unaonesha
kuwa rais Mkapa alipelekewa taarifa
kuhusu mchakato na kutoa
amri ya kuendelea
wakati tayari mkataba
ukiwa umeshafanyika na
kampuni imeshasamehewa kodi. Kwa
hiyo taarifa hiyo na
ruhusa ya Mkapa
ya kuendelea haraka
haikuwa na maana
yoyote.
Swali jingine lililojibiwa
na mahakama ni iwapo
msamaha wa kodi
ulikuwa halali kwa
kampuni hiyo.
Mahakama ilisema kuwa
ni kweli waziri
ana mamlaka kisheria
ya kusamehe kodi
lakini ikaongeza kuwa
mamlaka hayo yana
ukomo. Ikasema kuwa haimaanishi
kuwa kwa kuwa sheria
hiyo inamruhusu waziri asemehe kodi
basi atasemehe kodi kila
atakapojisikia kufanya hivyo
au akili yake
atakavyomtuma. Ikasema hata watuhumiwa
wanalifahamu hilo na
ndio maana walikuwa wakiomba
ushauri kuhusu jambo hilo
japo hawakuuzingatia. Ikasema
suala la kodi
ni suala la kiufundi si
la kuamuliwa kwa
utashi. Kwa nukta hiyo mahakama
ikasema hakukuwa na sababu
za kutoa msamaha
wa kodi kama watuhumiwa
walivyofanya.
Kuhusu tozo kubwa
iliyokuwa ikitozwa na kampuni
hiyo mahakama imesema
kuwa watuhumiwa napo walikataa
kuzingatia ushauri waliopewa
na wataalam pamoja
na utafiti uliofanyika
katika nchi nyingine
na kuona taifa
linanyonywa na kampuni
ya Alex.
Hoja kuwa serikali
haikupata hasara nayo
ilijibiwa . Mahakama ilisema
kwamba ni kweli
kodi iliyosamehewa kisheria
haiitwi hasara. Lakini
ikasema kuwa isiyoitwa
hasara ni ile
kodi iliyosamehewa kihalali
na kwa kufuata
utaratibu. Ikasema kuwa
kodi iliyosamehewa bila
uhalali na bila
kufuata utaratibu hiyo
ni hasara na hivyo
ni kweli watuhumiwa
waliliingizia taifa hasara.
Kwa hoja hizi Mramba
na Yona wakakutwa
na hatia.
11. KUACHIWA
HURU KWA
GRAY MNGONJA.
Sababu kubwa za
kuachiwa Mngonja ni,
kwanza wakati akiwa
katibu mkuu hakuwa
peke yake kwani walikuwepo
makatibu wakuu wengine
wawili yeye akiwa
watatu. Wote mmoja mmoja
kuna namna walivyoshiriki katika
mchakato huu na
hivyo kesi haikumgusa moja
kwa moja. Pili yeye
kama alivyojitetea alikuwa
akitekeleza maagizo ya
Mramba aliyekuwa bosi
wake na hakuwa
na namna ya
kukataa. Tatu hakuhusika katika
kusamehe kodi, hakuhusika katika kuongeza
muda wa mkataba na
wala hakuhusika katika kuipa
kampuni hiyo mkataba
mwanzoni. Yeye alipewa
maagizo ya kuandaa
matangazo ya serikali
ya msamaha wa kodi na
akafanya hivyo. Hii ndiyo pona yake
12. ADHABU WALIZOPEWA MRAMBA NA
YONA.
( 1 ) Mramba
alipatikana na hatia
katika kosa la
kwanza hadi la
kumi na moja .
Amehukumiwa kifungo cha
miaka mitatu kwa kila
kosa. Hata hivyo
mahakama imetoa amri
ya adhabu hiyo
kutumikiwa kwa pamoja
(concurrently) na hivyo kumfanya
Mramba kutumikia miaka mitatu tu
kwa ujumla badala ya
kila kosa miaka
mitatu.
Kosa la 11
atatakiwa kulipa faini
ya Tshs milioni
tano na akishindwa atumikie miaka mingine mitatu jela.
( 2 ) Katika
kosa la 1 -4 Daniel Yona
amehukumiwa kifungo cha
miaka mitatu kwa
kila kosa ambazo
zitatumikiwa kwa pamoja (concurently) yaani
miaka mitatu tu.
Kosa la 11
naye atalipa kiasi cha Tshs milioni
tano au akishindwa
atumikie miaka mingine mitatu jela. Hivyo
ndivyo ilivyotokea.