Swali langu hivi; Itakuawaje kama huyu mheshimiwa sana anayo team kubwa
kutoka huko chama tawala na wanahitaji nao kuyasaka mabadiliko nje ya ccm kwa
muda huu ambao tayari sasa mmeshapitisha wagombea wenu kwenye kura za maoni
Kufuatia mgawanyo wenu wa majimbo na huku nao wanazitaka nafasi hizo kupitia
UKAWA? Je,
Watakubali kubaki kua wasindikizaji tu? Wengine walikua ni wabunge
tayari kwa awamu iliyopita na bado ni watendaji wazuri na baadhi yao walikua
Mawaziri Watakubali kukaa bench?Je, hamuoni concentration ya Urais mnaipa
nafasi sana lakini huku Chini kunaweza kua na misuguano kikubwa? Je, hili suala
mnakabiliana nalo vipi mapema iwezekanavyo?