Mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu (hayupo pichani)
akinadi ilani ya Chama Cha Mapinduzi Jimbo la Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba.
Mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu kushoto akihutubia wanaCCM na wananchi babati Mjini.
Mbunge anaemaliza muda wake jimbo la Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba kabla ya mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu kupanda jukwaani kunadi sera za CCM.
Mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu akiwa jukwaani
akinadi ilani ya Chama Cha Mapinduzi Jimbo la Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba.
MGOMBEA mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia
Suluhu amesema chama hicho kikichaguliwa na Watanzania kuunda Serikali tena
kitahakikisha kinaweka utaratibu mzuri utakaomfanya mwananchi mfanyabiashara
kupenda kulipa kodi kwa ajili ya maendeleo. Samia ametoa ahadi hiyo Mjini Mbulu
alipokuwa akiwahutubia wananchi na wanaCCM katika mkutano wa hadhara wa kampeni
za chama hicho.
Alisema watahakikisha wanaondoa kodi za hovyo hovyo ambazo
zimekuwa zikitozwa hivi sasa katika maeneo.
"...Tutaweka utaratibu mzuri ambao utamfanya mwananchi
apende kulipa kodi, ila kodi za hovyo hovyo tutaziondoa...," alisema
mgombea huyo mwenza wa urais akiilani ilani ya CCM na kumuombea kura mgombea
urais wa chama hicho, Dk. John Pombe Magufuli.
Akihutubia mkutano mwingine Jimbo la Babati Mjini Bi. Suluhu
alisema serikali itakayoundwa na Chama Cha Mapinduzi ili kuboresha sekta ya
elimu itahakikisha inatoa elimu bure kuanzia darasa la kwanza hadi kidato cha
nne jambo ambalo pia litawapunguzia mzigo familia na kutoa fursa sawa ya elimu
ngazi ya msingi na sekondari (kidato cha nne).
Aidha alisema serikali itakayoundwa na CCM pia itahakikisha
inafanya maboresho makubwa katika sekta ya afya, umeme, huduma za maji safi na salama pamoja na
kuwawezesha wananchi hasa makundi ya vijana na akinamama.
Alisema katika maeneo ya wafugaji watahakikisha
wanashirikiana na halmashauri kupima na kuweka mipaka ya ardhi katika vijiji
ili kuondoa mvutano wa wakulima na wafugaji.
Kuwasaidia wafugaji
kujenga majosho ya nifugo ikiwa ni pamoja na ujenzi wa viwanda vya kuchakata
bidhaa za mifugo kuziongezea thamani.
Hata hivyo aliwahakikishia wanavijiji ambao wamekumbwa na
ukame kuwa Serikali imejipanga kuwasaidia hivyo hakuna mwanakijiji atakaye kufa
kwa njaa.
Pamoja na hayo
alisema Serikali ijayo ya CCM ili kuongeza kasi ya uwajibikaji imepanga kuunda
kitengo maalumu cha kupokea na kushughulikia kero na malalamikoa ya wananchi,
jambo ambalo litaweka bayana nani hataki kuwajibika kazini.