FIFA YAINGILIA KATI SAKATA LA MOURINHO NA DAKTARI WA CHELSEA

Shirikisho la Mpira wa Miguu duniani FIFA limepanga kujadili lile sakata la daktari wa Chelsea Eva Carneiro aliyechimbwa mkwara na kutolewa maneno machafu pamoja kufungiwa na kocha wa timu hiyo Jose Mourinho.

Caneiro alitolewa maneno makali na Mourinho baada ya yeye (Caneiro) na Jon Fearn kuingia uwanjani kumtibia Eden Hazard wakti Chelsea ilipolazimishwa sare ya goli 2-2 na Swansea ikiwa nyumbani Augost 8 mwaka huu.

Kitendo hicho kilisababisha Eden kutoka nje ya uwanja na kuwaacha wachezaji wa Chelsea wakibaki tisa uwanjani kufutia kadi nyekundu aliyooneshwa golikipa wa timu hiyo Thibaut Courtois.

Kamati ya madaktari ya FIFA itajadili sakata hilo kwenye mkutano wao Septemba 11 mwaka huu. Kamati inatarajia kutoa ushirikiano kwa madaktari wa timu wanaofanya kazi kuhakikisha wachezaji wanakuwa katika hali nzuri.

Mwenyekiti wa kamati hiyo Michael D’Hooghe amesema: “Huu ni mfano mwingine wa ugumu wa kazi kwa madaktari wa timu”.

“Nataka kujadili suala hili na wenzangu na kuona kama tunaweza kutoa tamko kusaidia madaktari wa timu”.


Mourinho alikosolewa baada ya mchezo huo kumalizika kutokana na sentensi aliyoitoa kuhusu madaktari wa timu yake kwenye uwanja wa Stamford Bridge lakini hakurudi nyuma wala hakuomba radhi.