Kampuni ya mafuta ya Utaliana, Eni, inasema imegundua katika
mwambao wa Misri, moja kati ya visima vikubwa kabisa duniani vya gesi.
Kampuni hiyo imesema kisima hicho kiitwacho Zohr, kiko mita
1,500 chini ya bahari, na inakisiwa kuwa kina mita za mjazo bilioni 850 za
gesi.
Mkurugenzi mkuu wa Eni amesema kisima hicho kipya kinaweza
kuwa mmoja kati ya ugunduzi mkubwa kabisa wa gesi duniani na kitasaidia kukidhi
mahitaji ya gesi ya Misri kwa miongo kadha ijayo.
Kampuni ya Eni ya Utaliana, ambayo ina haki kamili ya
kuchimba kisima hicho, ni kampuni kubwa kabisa ya kigeni Afrika katika sekta ya
mafuta na gesi.