Hali ya ugonjwa wa kipindupindu mkoani Morogoro imeendelea
kuwa tete baada ya idadi ya wagonjwa wa kipindupindu kungezeka hadi kufikia wagonjwa 45 ambao wanaendelea na
matibabu katika kambi maalum katika hospitali ya sabasaba mjini Morogoro.
Afisa afya mkoa wa Morogoro Carlesilas Lyimo amesema
kutokana na kasi ya ongezeko la kipindupindu maafisa afya wamefanya operesheni
katika maeneo mbalimbali yanayotoa huduma za chakula na vinywaji na kufanikiwa
kukamata na kumwaga pombe za kienyeji zaidi ya lita 770, kuwachukulia hatua
wafanyabiashara wa chakula wanauza vyakula bila utaratibu pamoja na kutoa dawa
za kuwakinga na kipindupindu majumbani kwa watu 410 wengi wao wakitokea kata ya
kilakala.
Nao wananchi wa mji wa Morogoro wameeleza wasiwasi wao juu
ya kuongezeka idadi ya wagonjwa wa kipindupindu ambapo wametupia mamlaka ya
maji safi na maji taka Moruwasa kushindwa kutoa
huduma ya maji kwa wananchi katika baadhi ya maeneo hali inayosababisha
wananchi kulazimika kutumia maji ya mito
ambayo si salama.