HII NDIO SHERIA YA MAKOSA YA MTANDAO, 2015

UTANGULIZI

Sheria hii ya makosa ya mtandao, 2015 imebainika kuwa na mapungufu
makubwa sana. Mapungufu hayo yamebainika kuwa, kama sheria ikipita
yanaweza kuifanya nchi ikawa ni kati nchi adui za matumizi ya mtandao
wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano duniani.

Watanzania wote wanatakiwa kufahamu kuwa muswada ukipita
utatumika nchini kote yani Tanzania Bara na Visiwani.

Watanzania walio wengi hawafahamu Sheria hii inawahusu kwa namna
gani; lakini kwa lugha rahisi ni kuwa itamuathiri mtu yeyote anayeweza
tumia mtandao wa intaneti kwa kutimia kifaa chochote iwe kompyuta
kubwa au vifaa vyenye uwezo wa kufanya kazi kama kompyuta kama
Simu za mikononi, saa, televisheni na vifaa vingine vinavyoendana na
hivyo.

Malengo ya Sheria hii ni kuainisha makosa yanayohusiana na matumizi
ya mfumo wa kompyuta na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano,
kuweka utaratibu wa upelelezi, ukusanyaji na matumizi ya ushahidi wa
kielektroniki na masuala mengine yanayohusiana na hayo.

Matumizi ya mitandao yote mikubwa kama Twitter, Instagram,
JamiiForums, Facebook, Barua pepe, WhatsApp, blogu na data zote
zilizo katika kifaa chochote cha kielektroniki yanaathiriwa kwa kiwango
kikubwa na Muswada huu.

UCHAMBUZI
Ibara ya 4
Ni computer gani inazungumziwa hapa? Ya nani?

Ibara ya 5
Computer gani inayokusudiwa, ya nani?

Ibara ya 7
(1-3): Haibainisha ni aina gani za data ambazo haziruhusiwi
kuguswa/kufutwa au zikiguswa/futwa ni kosa la jinai.

7(1g): Kipengele hiki katika ibara hii kinarudiwa mara kadhaa katika
(Ibara za 32-35). Badala ya ibara za mbele kurejea ibara hii, watunga
sheria wameiacha ibara hii ikiwa haieleweki hadi mtu asome ibara za
mbele.

Je mtu aliyeidhinishwa katika ibara na kipengele hiki ni nani?
Ibara ya 8:
Muswada huu haujaweka bayana iwapo nyaraka za siri zinaweza
kuwekwa wazi katika mtandao kama zina maslahi ya nchi au wananchi
mf. Matumizi mabovu ya pesa za umma

Ibara ya 14:
Neno pornografia halijapewa maana na hivyo jambo lolote lenye
mwonekano wa kiasherati (sexually vulgar) linaweza kutafsiriwa kama
pornografia na kumuingiza muhusika matatizoni.

Ponografia ya mtandao isikatazwe kabisa ila inatakiwa kuweka ulinzi
thabiti wa kuhakikisha watoto hawawezi kufungua mitandao ya aina
hiyo.

Ponografia zote ni chafu lakini sio chafu zote ni ponorafia. Hivyo
kutokana na kuwa sheria hii inasema ponografia zote ni chafu hii
itasababisha kila mtu ahukumiwe chini ya kifungu B.

Uchafu na Ponografia viwe vipengele viwili tofauti.
Artcile 15:
Suala la kujifanya mtu mwingine kwenye mtandao, linaweza kuleta utata
kwani kuna baadhi ya mitandao ambapo watumiaji hutumia majina
ambayo sio ya kwao. Itakuwaje watu kwa madhumuni mabaya wakitafuta
mtu mwenye jina kama hilo na kumshtaki mtumiaji wa mtandao?

Je, mtu kujifanya mtu mwingine inahusisha mtu kutumia jina lisilo lake
hata kama hajajifanya mtu mwingine? Ni vema suala hili likafafanuliwa
kisheria kwakuwa ni suala muhimu lakini wachache wataelewa manaa
yake.

Ibara ya 16:
Ni nani ana mamlaka ya kubainisha kuwa jambo lililowekwa kwenye
mtandao ni la UKWELI, UONGO au UPOTOSHAJI? Ni wazi kuwa
mamlaka husika inaweza tumia hili kama mtego kwa manufaa yao.
Kipengele hiki kama vingine kimeambatanisha muda usiopungua bila
kusema muda usiozidi. Hivyo mtuhumiwa anaweza kufungwa hata
kifungo cha maisha kutokana na mamlaka ya mahakama.

Watu binafsi wanaweza kutumia vibaya kifungu hiki kuzuia uhuru wa
maoni kwa kuwaburuza watumiaji wa mtandao mahakamani kila kukicha
na kuwapotezea muda wahusika ambao wanaweza kubainika mwishoni
kuwa walionewa.

Ibara ya 20:
Katika mawasililano ya mtandao kama ilivyo mawasiliano mengine kuna
ujumbe ambao mtu hawezi kuacha kuupata
Mfano kutembea barabarani na kuona bango la matangazo, au kuwa
ndani ya daladala iliyowasha redio.

Vivyo hivyo katika mtandao sio kila ujumbe anaopokea mpokeaji
ameuomba na hivyo kifungu hiki kinafanya kila mtu atakayepokea
ujumbe bila ridhaa yake kuwa amefanya kosa la jinai.

Ibara ya 21(1):
Tafsiri za Kiswahili na kiingereza zipo tofauti kabisa.
Ya Kiswahili inamlenga mtoa huduma na huku ya kingereza inamlenga
mtu yeyote anayetumia mtandao.

Ya Kiswahili inamlazimu mtoa huduma kumtaja mhusika aliyeweka
ujumbe na pia kumuadhibu mtoa huduma huku ya kiingereza
inazungumzia kuhusu tafiti kwa ujumla.

Ya kiingereza ni nzuri lakini ya Kiswahili imepotoshwa kabisa na
inavunja uhuru wa mawasiliano.

MUHIMU:
Hakuna kinga yoyote kwa mtoa taarifa (source) kwa mujibu wa ibara hii.

Ibara ya 22:
Je, nani ana mamlaka ya kuamua kuwa ujumbe kwenye mtandao
unatolewa au kuboreshwa kwa kusudi au bila kusudi.

Itambulike kuwa ujumbe wa kwenye mtandao huboreshwa (edit) au
kufutwa wakati wowote muhusika anapoona inafaa mf. Whatsap status,
fb status etc.

Ibara ya 23:
Unyayasaji wa kupitia mtandao (cyber bullying) haujapewa maana.
Sheria inatakiwa kuweka bayana maudhi ya kihisia ni nini.

Kwani mtu yeyote atakayeudhiwa ‘kihisia’ au kudai kuwa hisia zake
zimeudhiwa anaweza kushtaki. Sio kila linalosababisha maudhi ya kihisia
ni unyanyasaji

Ibara ya 27:
Ni nani anaamua kitendo fulani ni kula njama? Mazungumzo ya kawaida
na maamuzi ya kukubalika na upande mmoja yanaweza kutafsiriwa kama
kula njama na watu wa upande mwingine.

Ibara ya 31 (3a):
Sheria ya kiingereza inasema ‘as soon as practicable’ lakini ya
Kiswahili inasema wakati wa upekuzi na ukamataji wa mali. Hizi zina maana tofauti.

Ibara hii inawapa mamlaka Wakuu wa Vituo vya Polisi kufanya upekuzi
na kuchukua mali(za kielektroniki) na taarifa binafsi za raia bila amri ya
Mahakama.

Ibara ya 32-35
Ibara hizi zinamlazimisha mtoa huduma kutoa data za wateja wake kwa
Mkuu wa kituo cha Polisi bila kibali cha Mahakama. Wakuu wa Vituo
vya Polisi wamepewa nguvu sana katika sheria hii! Mahakama ipewe
mamlaka haya na si Polisi, na ifanyike hivi baada ya kujiridhisha kuwa
mwananchi anatakiwa kufanyiwa upekuzi, kuchukuliwa data zake au za
wateja wake n.k

Ibara ya 39-45
Watoa huduma na wahifaji tovuti wanalindwa na ibara hizi lakini kwa masharti.
Katika ibara ya 39, Waziri anapewa mamlaka ya kuamua kipi ni kosa na kipi si kosa.
Anapewa mamlaka ya kusimamisha na kusitisha huduma, kuondoa taarifa juu ya kitendo
husika (mfano kulazimisha kuondoa mijadala yote ya ufisadi flani kama yeye ataona kwa
mamlaka yake kuwa haufai kujadiliwa).

Muswada huu ibara za 31-38 na ibara za 39-46 zinakinzana kwani kwa wakati mmoja mtoa

huduma anaweza akawa ameona jambo ameshalitoa na anajiandaa kuitaarifu mamlaka husika

huku mamlaka husika (Askari Polisi) ikiwa na uwezo wa kwenda kuchukua vifaa na data za mtoa huduma.


Mamlaka ya Polisi imepewa kinga kubwa ambayo haiingiliani na sheria yoyote ile.