Jeshi la Nigeria
linasema kuwa limewaokoa zaidi ya watu 180, wengi wao wanawake na watoto,
kutoka kwa kundi hatari la wapiganaji wa kiislamu la Boko Haram, katika jimbo
la Borno.
Kupitia taarifa kwa vyombo vya habari, msemaji moja wa jeshi
amesema kuwa kambi kadhaa za waasi hao zilizoko karibu na mji wa Maiduguri zimeharibiwa na kamanda mmoja wa Boko Haram
kukamatwa, lakini duru hizo hazijasema ni lini tukio hilo lilifanyika.
Wakati hio huo, Rais wa Niger, Mahmadou Issoufou, amesema
kuwa jeshi jipya linalojumuisha wanajeshi kutoka mataifa kadhaa huko Afrika
magharibi, lina uwezo mkubwa wa kukabiliana na Boko Haram.
