YELEUWIII! Katika hali ya kushangaza, sauti ya mpenzi wa
staa wa muziki na filamu Bongo, Zuwena Mohamed ‘Shilole’, Naftal Mlawa ‘Nuh
Mziwanda’ inayosikika akimtongoza Wema Sepetu imemfikia Shilole na kusababisha
azimie
Nuh kajipambanua ileile. Kaimbisha mistari yote ya kimahaba,
utafikiri alikaririshwa. Alijitahidi kushusha vesi tamu ili kumuingiza Wema kwenye himaya yake. Huwezi
amini jamaa alizidisha mbwembwe kiasi cha kumwambia amkubalie kwani hamtaki
Shilole tena.
WEMA AMTOSA
“Wema amesikika akikataa, akamwambia hawezi kuwa naye kwani
ni shemeji yake na anamheshimu Shishi,” kilisema chanzo hicho.
SHILOLE AMFUATA NUH
Chanzo hicho kilieleza kuwa, baada ya kuusikiliza ujumbe
huo, Shilole alimfuata Nuh kwa ajili ya kumsikilizisha lakini Nuh alijibu
‘mbovu’ ndipo Shilole alipomuomba ufunguo wa gari waliyokwenda nayo, akarudi
alipokuwa amekaa awali.
APOTEZA ‘NETIWEKI’
“Aliporudi alipokuwa amekaa, Shilole alijikuta akiishiwa
nguvu na kuzimia ambapo Aunt Ezekiel na kina JB (Jacob Stephen) walipofanya
kazi ya ziada kumpepea, huku wengine wakihangaika kummwagia maji kunusuru afya
yake.
“Walifanikiwa kumpandisha kwenye gari lake. Joto lilikuwa
kubwa kufuatia hali hiyo maana kila mtu alishindwa kuelewa kilichotokea, hivyo
Shilole, baada ya kuzinduka aliulizwa kilichomfanya azime ambapo
aliwasikilizisha sauti hiyo kila mmoja akabaki ameduwaa,” kilieleza chanzo.
AUNT AOKOA JAHAZI
Ilielezwa kuwa, mwigizaji Aunt Ezekiel ndiye aliyeokoa
jahazi kwa kulazimika kuendesha gari la Shilole na kumpeleka nyumbani huku Nuh
akipandishwa kwenye gari la JB kumpeleka kwa ndugu zake.
MSIKIE SHILOLE
Paparazi wetu, baada ya kupenyezewa ubuyu huo, alimtafuta
Shilole ili kupata habari kamili ambapo alikiri kupokea ujumbe huo wa sauti
huku akiainisha kuwa umemkera kwani kuna maneno yanasikika akimponda yeye.
“Inaniuma sana ,
Nuh kuendelea kunidhalilisha kiasi hicho wakati ni mwanaume ambaye ninamheshimu,
tunakoelekea uzalendo utanishinda.
“Nilipousikiliza ujumbe ule kwa mara ya kwanza sikuamini
nilichokisikia. Pamoja na Wema kuonesha wazi msimamo wa kumkataa Nuh ila mimi
naona kama fedheha kubwa kwangu kwani ninamheshimu sana .
“Watu wananiona mimi mkorofi lakini kama
ningekuwa napenda kuweka kila jambo wazi, hakuna mtu angeendelea kunifikiria
vibaya.“Siwezi tena kuendelea kuumiza moyo wangu kila kukicha,” alisema Shilole
ambaye anatumikia kifungo cha Basata kwa kutojishughulisha na sanaa kwa
takriban mwaka mmoja kwa kosa la kucheza nusu utupu jukwaani.
