Ikiwa ni siku Chache tangu lowassa ajiunge na chama cha
chadema kumekuwepo uvumi kuwa MBUNGE wa Ubungo, John Mnyika, amekiama chama
chake kutokana na chama hicho kumkalibisha Lowassa na kumpa nafasi ya juu
kabisa
Ukweli wa madai haya umethibitishwa leo hii baada ya Mnyika
kuhudhulia katika mkutano wa kamati kuu (CC) ya chama cha demokrasia na
maendeleo
Taarifa kutoka ndani ya kikao cha CC kinachofanyika katika
hoteli ya Bahari Beach zilizotufikia dawati la habari clansmedia zinasema,
Mnyika amehudhuria mkutano huo na kueleza kuwa kutoonekana kwake, kumetokana na
matatizo ya kifamilia.
Mwanasheria mkuu wa Chadema, Tundu Lissu amethibitisha
Mnyika kuhudhuria mkutano huo.
“Mnyika yupo ndani ya ukumbi wa mkutano. Anashiriki kikao
cha kamati kuu. Waliokuwa wanadhani chama chetu kimepata mpasuko kutokana na
ujio wa Lowassa, walikuwa wanajidanganya.” alisema Lissu
Lissu amesema, ndani ya Chadema wako wamoja, yote
yaliyotokea yalikuwa mapambano yanayotokana na ukomavu wa kidemokrasia uliyopo
Endelea kutufatilia kwa kila habari inayofika juu ya dawati letu la clansmedia..