Mradi mkubwa wa kuzalisha nishati kwa kutumia biogesi au
gesi viumbe umeanza kufanya kazi kusini magharibi mwa Kenya , miaka mitatu baada ya ujenzi
wake kuanza.
Mradi huo wa kwanza kabisa wa aina yake barani Afrika
umejengwa mjini Naivasha na una uwezo wa kuzalisha megawati 2.6 za umeme na
utaunganishwa na gridi ya taifa na kufanya gharama ya umeme zishuke zaidi.
Mradi huo wenye thamani ya dola za kimarekani milioni 7.5, utapunguza gharama
ya serikali inayotokana na manunuzi ya mafuta kwa ajili ya kuendesha mitambo ya
kuzalisha umeme.
Gavana wa Kaunti ya Nakuru Kinuthia Mbugua amesema mradi huo
utapunguza uchafuzi wa mazingira na kuokoa gharama za kununua lita milioni tano
za diseli ambazo hutumika kuzalisha kiwango cha umeme kama
huo kila mwaka.