LOWASSA: Nikiwa Rais Nitamtoa Babu Seya na Mashehe wa Kiislam Walioko Jela.

Leo Jagwani Katika Uzinduzi wa Kampeni za Ukawa Lowassa Amewagusa Wengi baada ya Kuzungumzia Suala la Babu Seya ambaye yupo jela amefungwa kifungo cha Maisha yeye na mtoto wake ..Lowassa Amesema kuwa amesikia kilio cha wengi kutaka aachiwe huru hivyo atakapo ingia madarakani atalitazama swala hilo.

Pia Lowassa Ameongelea kuhusu Mashehe wa Kiislam ambao wako Mahabusu na wengine Jela nakusema kuwa atashughulikia endapo atapewa nafasi ya kuwa Rais.