Makumi ya Wasichana Wafaridi Dunia Swaziland

Wasichana wasiopungua 38 wamefariki dunia katika ajali ya barabarani wakiwa njiani kwenda kumchezea Mfalme Muswati III wa Swaziland katika sherehe za kila mwaka zinazowashirikisha maelfu ya wasichana ambao mfalme huyo huchagua mke wake mpya baina yao.

Vyombo vya habari nchini Swaziland vimeripoti kuwa wasichana hao wamepata ajali barabarani baada ya basi lao kugongana na gari jingine. Wasichana hao walitazamiwa kushiriki katika sherehe ya kesho Jumatatu ambapo makumi ya maelfu ya wasichana bikira watashiriki na kucheza mbele ya Mfalme Muswati III kabla ya kuchagua mmoja wao kuwa mke mpya. Mflme Muswati III ameitaja ajali hiyo kuwa ni maafa ya kitaifa.
Vyombo vya habari vya Swaziland vimezuiliwa kupiga na kuonesha picha za ajali hiyo.

Mfalme Muswati III mwenye umri wa miaka 47 ana baina ya wanawake 13 na 15.