Kipindupindu ni ugonjwa wa ghafla wa
kuhara unaosababishwa na kula chakula au kunywa maji/vinywaji vyenye vimelea/ bakteria
waitwao Vibrio cholera . Watafiti wanakadiria
kuwa kila mwaka, kuna kesi
takribani milioni 1.4-4.3 na vifo
28 000-142 000 vinavyotokana na ugonjwa wa Kipindupindu. Muda mfupi wa maambukizi ni sababu moja wapo ambayo husababisha kuenea kwa mlipuko wa
kipindupindu.
Mtu hupata maambukizi ya kipindupindu baada ya kutumia
chakula au maji yaliyo chafuliwa na kinyesi cha mtu mwenye vimelea wa
kipindupindu. Vifuatavyo ni vyanzo vya maambukizi
•Vyanzo vya maji yaliyochafuliwa na kinyesi cha binadamu
•Barafu zilizotengenezwa kutokana na maji machu
•Vyakula au vinywaji vinavyouzwa mtaani
•Mbogamboga ambazo zinamwagiliwa maji yaliyochafuliwa na
kinyesi cha binadamu
•Kula samaki wabichi au ambao hawakuiva vizuri na wametoka
katika maeneo ambayo yanachafuliwa na kinyesi cha binadamu.
Dalili za Kipindupindu
Kipindupindu ni ugonjwa wa hatari sana .
Dalili hujitokeza kati ya masaa mawili
mpaka siku tano baada ya kupata maambukizi.
Ugonjwa huu huathiri watu wa rika zote watoto na watu wazima.
Kipindupindu kinaweza kuua ndani ya
masaa machache baada ya dalili
kujitokeza.
Asilimia 80 ya watu
walioambukizwa vimelea wa kipindupindu hawaonyeshi dalili yoyote.Hata
hivyo mtu ataendelea kutoa bakteria katika kinyesi
chake kwa muda wa siku 1-10 baada ya kuambukizwa na hivyo kusababisha
bakteria hao kusambaa katika mazingira
hivyo kuongezeka uwezekano wa
kuwaambukiza watu wengine.
Miongoni mwa watu ambao huonyesha dalili, 80% huwa na dalili
kiasi au wastani, wakati 20% wana
harisha majimaji kwa wingi na kupata upungufu mkubwa wa maji mwilini. Hali
isipotiwa huweza kusababisha kifo.
Maambukizi ya Kipindupindu
yana mauhusiano ya karibu na
usimamizi duni wa mazingira. Mfano
maeneo ambayo yako katika hatari ni makazi duni pamoja na maeneo
yaliyoko kandokando mwa miji, ambapo miundombinu ya msingi haipatikani, na pia
maeneo ya makambi ya wakimbizi, ambapo mahitaji ya kimsingi ya maji safi na
usafi wa mazingira ni hayapatikani kwa urahisi.
Migogoro katika
jamii uhaba wa mifumo ya maji na
usafi wa mazingira, Makambi ya wakimbizi au makazi yenye msongamano mkubwa wa
watu inaweza kuongeza hatari kuenea
kwa maambukizi ya kipindupindu
Kipindupindu bado ni
tishio duniani kwa afya ya umma na ni
kiashiria muhimu cha ukosefu wa maendeleo ya kijamii.
Matibabu
Kipindupindu ni ugonjwa ambao unatibika urahisi . Asilimia
80 ya wagonjwa wanaweza kutibiwa kwa ufanisi kwa kutumia dawa za majimaji (WHO / UNICEF ORS) .
Wagonjwa wenye upungufu mkubwa wa maji mwilini huitaji kuongezewa maji ya drip
kwa njia ya mshipa. Wagonjwa hawa pia
huitaji antibiotics sahihi ili kupunguza muda wa kuhara, kupunguza kufupisha
muda wa bacteria wa kipindupindu kutolewa kwenye kinyesi.
Hata hivyo, unaweza kujikinga wewe pamoja na familia yako
kwa kutumia maji ya chupa ,maji ambayo yamechemsha, maji ambayo yametiwa
kemikali ya kuwa vijidudu.Hakikisha kuwa
unatumia maji ya chupa, kuchemsha, au yaliyotiwa kemikali kwa madhumuni
yafuatayo:
•Maji ya kunywa
•Kuandaa chakula au
vinywaji
•Kutengeneza Barafu
•Kuosha vyombo vya chakula
•Kuosha matunda
•Kupiga mswaki