Wananchi wa eneo la Misugusugu Wilayani Kibaha Mkoani Pwani
hii leo wamefunga barabara baada ya Wanafunzi wawili kugongwa na gari la Jeshi
la Polisi na kupelekea kifo cha Mwanafunzi Mmoja.
Akiongea na Mtandao huu, Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa
Pwani Jaffary Mohammed amesema baada ya tukio hilo Wanachi walifunga barabara
kutokana na hasira ya tukio lakini jeshi la Polisi limetuliza hali na linamshikilia
Dereva wa gari hilo kwa uchunguzi zaidi.
Kamanda Jaffary ameongeza kuwa katika tukio hilo Mwanafunzi
aliejeruhiwa amelazwa katika hospitali ya Tumbi na mwili wa marehemu upo
mochwari katika hosptali hiyo.
Aidha Jaffari ameongeza kuwa kwa sasa hali ya kiusalama
imetulia baada ya jeshi la polisi kutuliza hali iliyojitokeza huku akiwataka
wananchi kuacha kujichukulia sheria mikononi na badala yale wafuate sheria.
Katika hatua nyingine amewataka madereva wafate sheria za
barabarani kwa kufuata alama zilizowekwa pamoja na kupunguza mwendo katika
maeneo ya watu ili kuepusha ajali zinazoweza kuepukika.