SHERIA mpya ya
Makosa ya Mtandao ya mwaka 2015 na
Sheria ya Miamala ya Kielektroniki ya mwaka 2015 zitaanza kutumika rasmi kesho
Septemba Mosi mwaka huu, hivyo watumiaji
na watoa huduma waaswa kuzingatia sheria hizi ili kuepuka mkondo wa
sheria.
Kauli hiyo imetolewa
leo na Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa
wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dares Salaam kwenye ukumbi wa
mikutano wa wizara hiyo.
“Sheria hizi ni nzuri zitaanza kutumika Septemba Mosi mwaka
huu,kuanzia saa 6.00 usiku . zina maslahi katika nchi yetu. Ninatoa wito kwa
wananchi kuzingatia matumizi salama ya mtandao kwa manufaa yako na maendeleo ya
Taifa letu,” alisema Profesa Mbarawa.
Aliongeza kuwa sheria hiyo ya makosa ya mtandao ya mwaka
2015 hazihitaji utungaji wa kanuni kwa kuwa iko wazi.
Alisema tayari
wizara imeanza kuelimisha watu kuhusu sheria hiyo na itendelea kuwajengea uwezo
wadau mbalimbali.
Profesa Mbarawa alisema sheria ya makosa ya mtando ya mwaka
2015 na Tanzania sio nchi ya
kwanza kuwa nayo, bali nchi mbalimbali zina sheria kama hiyo ,ambapo alitolea
mfano Uingereza ,India ,Malaysia , Uganda
na Korea
ya Kusini.
Akizungumzia kuhusu
madai sheria hiyo kuhusika na suala la Uchaguzi Mkuu, alisema si kweli,
bali imekamilika katika kipindi hicho ndio maana baadhi ya watu wanadai
hivyo.Aliongeza kwamba sheria hiyo imetunga ili kudhibiti matumizi ambayo si mazuri.
“ Mtu akitumiwa ujumbe akiupokea hapaswi kuisambaza kwani atakapousambaza atakuwa na amefanya
kosa,” alisisitiza.
Aliyataja baadhi ya makosa kuwa ni usiri, usalama wa
upatikanaji wa taarifa za kompyuta na mifumo
kama vilekuingilia mawasiliano ya
kompyuta au mifumo ya kompyuta kinyume cha sheria na wizi wa taarifa kimtandao.
Makosa dhidi ya
kompyuta ikiwa ni pamoja na,udanganyifu kwa kutumia kompyuta,kugushi kwa
kutumia kompyuta wizi wa utambulisho wa mtu binafsi mtandaoni, matumizi ya vifaa kinyume cha
sheria.
Makosa yanayohusiana
kimaudhui kama vile usambazaji wa ponografia,
ponografia za watoto makosa dhidi ya ubaguzi wa rangi na chuki, michezo ya
kmari mtanadaoni kiunyume cha sheria, kashfa na habari za uongo na makosa dhidi
ya haki na hati miliki.
Pia inatambua muungano wa makosa inajumuisha kama vile utakatishaji wa fedha haramu na ugaidi kwa
kutumia mtandao.