HATIMAYE Mahakama kuu
imelifungua rasmi Gazeti la Mwanahalisi ambalo lilifungiwa na serikali kwa mda
usiojulikana .Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo.
Akizungumza na Fullhabari.blogs, Mhariri wa Gazeti la
Mwanahalisi ,Jabir Idrisa amethitisha kuwa Jaji wa mahakama kuu Salvatory
Bongole,amelifungulia Gazeti hilo na kulitaka liendelee na kazi yake ya
kuhabarisha umma baada kubainika katika
kulifungia kwake kanuni zilikiukwa.
Amesema hukumu hiyo imetokana na kesi namba 27 ya mwaka 2013
ambapo Kampuni ya Hali halisi limited
ambao ni wachapishaji wa Gazeti la Mwanahalisi walikuwa wakitaka patio
la hatua ya waziri wa Habari Fenera Mukangala juu ya kulifungia Gazeti hilo, Katika kesi ambayo iliwakilisha
kwa Upande wa Serikali na ofisi ya Mwanahseria mkuu wa Serikali.
Jabir amesema Mahakama imebaini waziri wa Habari
hakufuata sheria katika kulifungia
gazeti hilo ,licha
ya kuwa na mamlaka ya kutokana na sheria ya Kandamizi ya Magazeti ya mwaka 1976 inampa uwezo wa kulifungia gazeti,
Amesema Sheria iyo inamtaka waziri husika kufuata hatua
kabla ya kulifungia Gazeti ambapo hatua hiyo ni kuwafuata wale anawaowatuhumu
ili wapate utetezi na kuchukua hatua lakini waziri huyo alipolifungia Gazeti hilo hakufuata hatua hizo.
HATUA GANI INAFUATA
BAADA YA HUKUMU HIYO.
Mwandishi huyo mwandamizi amesema kwa sasa kinachofuata ni
kutaka fidia toka serikalini juu ya hasara iliyopatika wakati Gazeti hilo lilipokuwa
limefungiwa huku akisema mahakama imeamulu wafanye hivyo.
Amesema Chengine kinachofuata ni mwenyewe Mmiliki wa Gazeti hilo akiamua kuchapisha Gazeti hilo
anachapisha au aache kutokana na
mahakama hiyo kumruhusu.
Kufunguliwa huko kwa Gazeti la kiuchunguzi la Mwanahalisi
kunakuwa ni kama ushindi kwa Mkurugenzi wa Gazeti Saed Kubenea Mara kwa mara
amekuwa ikidai serikali kulifungulia Gazeti hilo kimakosa.