Televisheni au runinga (pia: TV, telly au tyubu) ni
chombo (kifaa) chenye kiwambo au kioo ambacho kinapokea mawasiliano kutoka
katika kituo cha televisheni na kuyabadilisha kuwa picha na sauti. Neno
"televisheni" linatokana na neno tele (kutoka Kigiriki: kwa mbali
sana) na Kilatini vision (kuona), kwa pamoja inaunda neno tele-visheni.
Historia ya televisheni
TV ya Kijerumani ya mwaka wa 1956
TV ya Kijerumani ya mwaka wa1959
Kikawaida TV inaonekana kama sanduku. TV za zamani kabisa
zilikuwa zina kirimba au fremu kubwa ya mbao na zilikuwa zikiwekwa chini kama
fanicha. TV za kisasa ziko za namna nyingi kama zilivyo nyingi zaidi. Kuna
baadhi ya TV zinaweza kunea mkononi mwako na zikawa zinaendeshwa kwa kutumia
mabeteri.
TV zingine zinaweza kuenea ukuta mzima wa nyumba, na
inaweza kukaa katika sakafu, au kuna zingine ambazo zimenyooka (flat) na
zinaweza kubandikwa ukutani. Televisheni inaweza kuonyesha picha kutoka sehemu
mbalimbali. Cha kwanza unachotakiwa kufanya ni kutumia kidaka mawasiliano au
antenna (au aerial), hii itaonyesha maonyesho yote yanayorushwa na kituo cha
matangazo ya televisheni.
Vituo vya TV vinaweza kuwa mbali kabisa lakini bado
matangazo yake yanapatikana kama antena ya kurusha mawimbi yake iko katika
umbali wa kilomita 50 hadi 150. Teknolojia mpya zaidi ni kutumia vyombo vya
angani kama antena ya kurusha mawimbi haya duniani. TV pia inaweza kuonyesha
filamu kutoka katika VCD na DVD au VCR yaani tepu za kawaida. Cable TV na
Satellite TV zinaweza zikatoa huduma nyingi ya vipindi vya TV kwa mara moja na
vilevile kuvirusha hewani. Michezo mingi ya Video huunganishwa katika TV ili
uweze kuona kile unachokicheza. Kuna baadhi ya tarakilishi au kompyuta ambazo
unaweza kutumia TV kama kioo cha kufanyia kazi zako (kiwambo) au kwa jina
lingine monitor.
TV zote zina kiwambo ambacho kinaonyesha picha. Kabla ya
miaka ya 1970 TV zilikuwa hazina rangi ( yaani "black and white"),
ambazo zilikuwa zinafanya kila kitu kionekane cha rangi ya kijivu. Lakini kwa
sasa karibuni TV zote zinaonyesha na rangi. Kawaida ya viwambo vingi (kioo au
vioo) vingi huonyesha kuwa vina kona ya mzunguko, lakini kwasasa vioo vingi
hutengenzwa kwa kunyooka na zina ncha pembeni.
Njia ya picha katika TV
Kabla ya miaka ya 1990, TV zote zilikuwa zikitengenezwa
kwa umbo moja-zilikuwa kubwa kidogo na kisha zilikuwa ndefu. Kwa mfano, kama
kioo kilikuwa cha urefu wa inchi 3, basi lazima kitakuwa na upana wa inchi 4.
Au kama kioo kina urefu wa cm 30, lazima kitakuwa kina upana wa cm 40.
Umbo la TV za kisasa linazidi kuwa maarufu na kupata
wapenzi wengi zaidi kila siku ziendapo. TV zenye kioo cha upana mkubwa wa
mstatili huonekana vizuri katika runinga kubwa (theatre screen) na pia
inapendeza wengi zaidi. Hizi huziita kioo kipana (au kwa kiing: widescreen).
Endapo TV ya kioo kipana ina urefu wa cm 30, basi lazima itakuwa ina upana wa
cm 53. Ili ifanye kazi vizuri, uonyeshaji wa TV pia unatakiwa ujengwe kwa namna
ya upana yaani 'widescreen'. Kioo kipana kinaweza kubadilishika kwa ukubwa
wowote unaoutaka, lakini swala la umbo linabaki kuwa vilevile kama lilivyo
(Widescreen).