utapika ni dalili inayojitokeza kwa mama mjamzito hasa
kipindi cha awali ingawa tatizo la kutapika au kuhisi kichefuchefu linaweza
kutokea katika maradhi mengine mbali mbali tofauti na ujauzito.
Hali ya kutapika kwa mama mjamzito imegawanyika katika
makundi mawili.Kwanza ni kichefuchefu na kutapika wakati wa kipindi cha mwanzo
cha ujauzito ( Early pregnancy) na pili ni kipindi baada ya hicho cha awali
(Late pregnancy).
Morning sickness.
Tatizo hili hujitokeza
miezi ya awali ya ujauzito. Mara
nyingi haziendelei baada ya wiki ya 12. Mama anakuwa na kichefuchefu na anaweza
kutapika hasa wakati wa asubuhi.
Hyperemesis
gravidarum
Tatizo hili linaambatana na mama kuishiwa maji mwilini
kwa kutema mate,kutapika na kushindwa kula na wakati mwingine hulazwa
hospitali,
Kutapika kunakoendelea wakati wa ujauzito (late pregnancy)
huwa ni muendelezo wa hali hiyo.Tangu mwanzoni hali ya awali (Early pregnancy)
hutokea mimba inapokuwa chini ya miezi minne lakini hii hali ya pili ‘Late
pregnancy inatokea mimba inapokuwa zaidi ya miezi minne.Hapa mama huendelea tu
kutapika na vilevile inahusiana na dalili za magonjwa mengine kama
dalili za awali za kifafa cha mimba.
Yapo magonjwa mengine yanayosababisha kichefuchefu na
kutapika ambayo yanaweza kumpata mama mjamzito na asiye mjamzito.
Magonjwa haya ni kama vile minyoo, maambukizi ya njia ya
mkojo(Urinary Track infections),magonjwa ya ini(Hepatitis),ugonjwa wa kisukari
(pale sukari inapokuwa juu) (Ketoacidosis of Diabetes),mkojo kuingia katika
mfumo wa damu(uraemia),ugonjwa wa kidole tumbo (Appendicitis),vidonda vya tumbo
(peptic ulcer) kuziba kwa tumbo (Intestnal obstruction) matatizo ya nyonga
kifuko cha mayai (Twisted Ovarian cyst) na uvimbe katika kizazi (uterine
fibroid).
Inaaminika kutapika
kunasababishwa na kuongeza kwa hormoni ya eostrojeni. Baadhi ya akina mama
wanaotumia vidonge vya majira hupata dalili kama
za mama mjamzito. Pia hormone ya HCG inaweza kusababisha tatizo hil
Tatizo hili linaweza kutokea katika mimba ya kwanza
tu,wengine hutokea ya pili au wengine hutokea mimba zote.
Hali ya kisaikolojia (psychogenic) pia huchangia kuamsha
kichefuchefu kwa kutotamani baadhi ya vitu au vyakula au harufu.
Mama akiwa na hali hii hasa vyakula vya wanga hasa nyakati
za usiku,asubuhi ataamka na njaa na kichefuchefu na kuanza kutapika na kuchoka
Chakula cha wanga kama wali na ugali ni muhimu kwani vinatia
nguvu na joto,vilevile uwepo wa vitamini B za kutosha nao husaidia sana .
Tatizo hili la kichefuchefu na kutapika pia huchangiwa na
mzio (Allergies ) mbalimbali na tumbo kutofanya kazi vizuri (Decreased gastric
motility).
Ufanye nini
Mara nyingi kichefuchefu cha kawaida hakiitaji tiba
yoyote.Hata hivyo kichefuchefu kikali zaidi kinaitaji matibabu ya haraka. Hivyo
ni vyema ukiwahi hospitali.
Matibabu
Matibabu hutegemea dalili. Hata hivyo mgonjwa anaweza
kuongezea maji na kupewa daw za kuzuia kichefuchefu pamoja na kutapika.
Pia ni vyema mgonjwa akijitahidi kula hasa vyakula vya jamii ya wanga pale
anapopata nafuu. Maji ni muhimu. Tena mara kwa mara. Hii itasaidia kupunguza
uwezekano wa upungufu wa maji iwapo hali itajiru