Ipo haja kubwa sana
ya kujifunza kupitia watu waliofanikiwa ili kuweza kufikia mafanikio mkubwa.
Kupitia maisha yao
kuna mambo mengi ya msingi tunakuwa tunajifunza na kuachana na makosa ambayo
wao waliyafanya bila kujua.
Na kiuhalisia yapo mambo mengi ya kujifunza kutoka kwa watu
waliofanikiwa ambayo yanaweza kuwa msingi mkubwa wa mafanikio yetu. Kuyajua
mambo hayo itakusaidia kujiamini na kuendelea mbele. Mambo hayo ya kujifunza
kutoka kwa watu waliofanikiwa ni kama haya
yafuatayo:-
2. Watu waliofanikiwa ni watu wa kuishi kwa bajeti. Mara
nyingi hujikuta wakikata au kupunguza kile ambacho siyo cha muhimu katika
bajeti yao na
kutengeneza bajeti upya itakayowafanikisha. Kwa kifupi, matumizi yao kwa sehemu kubwa
yanaongozwa na bajeti.
3. Watu waliofanikiwa ni watu wa vitendo. Mara nyingi siyo
waongeaji sana .
Ni watu wa kuchukua hatua ambazo zinaleta matokeo halisi na chanya
yatakayojitokeza kwenye maisha yao .
4. Watu waliofanikiwa wako makini na suala zima la
uwekezaji. Kila wakati wanafungua macho yao
kuangalia ni wapi ambapo wanaweza kufanya uwekezaji ambao utawaletea matunda na
mafanikio makubwa badala ya kukaa na kutumia pesa hizo tu.
5. Watu wenye mafanikio wanatumia muda wao mwingi kujifunza.
Kwa kifupi hawa ni watu wa kujifunza kupitia vitabu mbalimbali wanavyovisoma
hata pia kuhudhuria semina au warsha za mafanikio.
6. Watu wenye mafanikio ni watu kuendelea mbele hata pale
inapotokea wameshindwa katika jambo fulani. Huwa hawasimami kusikilizia sana maumivu hayo.
Hujifunza pale walipokosea na kisha safari ya mafanikio kuendelea kama kawaida.
7. Watu wenye mafanikio mara nyingi wanazungukwa na watu
wenye mitazamo chanya kama ya kwao. Watu hawa
wanaowazunguka huwasaidia zaidi kimtazamo na kuwafanya wawe na mafanikio muda
wote.
8. Watu wenye mafanikio hawana kauli za kushindwa kwenye
maisha yao .
Muda mwingi wamebeba kauli za mafanikio. Hutaweza kuja kuwasikia wakisema
‘siwezi hili, au lile’ badala yake hukaa na kusema ‘nitaweza vipi kufanya jambo
hili nakufanikiwa’ hizo ndizo kauli za watu wenye mafanikio siku zote.
9. Watu wenye mafanikio ni watu wa kujitoa mhanga. Siku zote
wako tayari kufanya na kutoa chochote ili mradi tu mipango na malengo yao yaweze kutumia na
kufika kule wanakotaka kufika.
10. Watu wenye mafanikio ni watu wa kufanya mambo yako kwa
kuweka nguvu nyingi za uzingativu katika eneo moja. Kama
kuna jambo wameamua kulifanya wanaling’ang’ania hilohilo mpaka liwape matokeo
kamili.
11. Watu wenye mafanikio ni watu wa kutunza muda siku zote.
Hawako tayari kupoteza muda wao kwa kufatilia mambo ambayo wanaona hayana
msaada kwao.
12. Watu wenye mafanikio ni watu wenye uvumilivu wa kutosha.
Kuna wakati huwa wanashindwa katika mambo yao ,
lakini huvumilia mpaka kuweza kufanikiwa.
Yapo mambo mengi sana
ambayo unaweza kujifunza kupitia watu waliofanikiwa, lakini unaweza ukayafanyia
kazi mambo hayo kwanza ili yawe msingi
bora katika safari yako ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa.