Matumizi mazuri ya muda ni moja kati ya changamoto kubwa sana inayotukabili wengi
wetu. Mara nyingi imekuwa ikitokea kwa wengi wetu karibu kila siku, kujikuta
tuna mambo mengi ya kufanya ukilinganisha na muda tulionao. Kutokana na mambo
hayo kuwa mengi, mipango yetu mingi pia hujikuta imekwama na kushindwa
kuendelea kutokana na ukosefu wa muda.
Lakini hata hivyo, pamoja na changamoto zote hizo za ukosefu
wa muda, kwa wengine bado hubaki kuwa ni watu wa kupoteza muda katika maisha yao . Nikiwa na maana kuwa,
wanakuwa ni watu ambao hawajali sana
kupoteza muda wao na pia hata wanakuwa wanawapotezea wengine muda hivyohivyo.
Najua umeshawahi kuwaona watu wa namna hii katika maisha yako wasiojali thamani
ya muda.
Hawa ni watu ambao huishi maisha yasiyo na mafanikio sana kutokana na kupoteza muda mwingi sana
katika maisha yao .
Kitu cha muhimu hapa kujua ni kuwa muda ni kitu cha thamani sana
kuliko kitu chochote duniani. Mafanikio yote yanategemea muda. Unapopoteza muda
wako ni sawa na kupoteza mafanikio yako. Sasa jiulize kama
wewe unapoteza muda unategemea nini katika maisha yako?
Ili uweze kufanikiwa na kuwa tajiri ni lazima kujifunza
kutumia muda wako vizuri tena sana .
Watu wote wenye mafanikio makubwa ni watumiaji wazuri wa muda wao kuliko
unavyofikiri. Kinachowatofautisha wao na wewe ni matumizi ya muda tu na sio
kitu kingine. Hiyo yote inaonyesha siri kubwa ya mafanikio ipo kwenye muda.
Kitu kingine cha kujiuliza tena je,
unataka kutunza muda wako na kujijengea mafanikio ya kudumu? Kama
jibu ni NDIYO.
1. Weka vipaumbele
vya kila siku.
2. Jiwekee malengo.
3. Fanya mambo
machache kwa uhakika.
Ni rahisi sana kwako kupoteza
muda kama utajikuta unataka kafanya mambo
mengi kwa wakati mmoja. Hii ni kwa sababu utashika hiki mara kile na kujikuta
hakuna ulichokifanya zaidi ya kurukaruka. Ili
kufanikiwa jifunze kufanya mambo machache kwanza ikiwezekana jambo moja tu.
Hiyo itakupa ufanisi wa kutunza muda wako vizuri sana .
4. Weka kumbukumbu ya
muda wako.
5. Kuwa makini na
mambo yanayokupotezea muda.
Kuna mambo ambayo wengi wetu huwa yanatupotezea muda bila
sababu. Jiulize ni kitu gani ambacho kinakupotezea muda sana . Je, ni mitandao ya kijamii, simu, mpira
au ni kitu gani? Ukishajua kitu kinachokupotezea muda sana , tafuta njia nzuri namna ya kupunguza
matumizi hayo. Acha kupoteza muda wako hovyo kwa kitu ambacho hakikupi faida ya
moja kwa moja, badala yake linda na tunza sana
muda wako kwani hapo ndipo mafanikio yako yalipo.
6. Jifunze kusema
HAPANA.
Wengi huwa wanajikuta ni watu wa kupoteza muda wao pengine
kutokana na kukubali vitu vingi bila kujiuliza kwa nini walikubali. Kabla
hujasema ndiyo kwa jambo lolote la makubaliano jiulize linawezekana? Kama hutajifunza kusemaHAPANA hii itakufanya uzidi
kupoteza muda wako mwingi wa thamani siku hadi siku bila ya wewe kujua. Kama huelewi kitu ni bora ukasema HAPANA kuliko ukafanya
na ukaacha, hiyo itakuwa ni kupoteza muda.
7. Wape wengine
majukumu.
Kama pengine kuna jambo ambalo unataka kulifanya wewe,
lakini ukagundua wapo watu ambao wanaweza wa kakusaidia katika jambo hilo ni vizuri ukawapa
wakafanya. Hiyo itakusaidia kufanya majukumu mengine zaidi na isitoshe utakuwa
umeokoa muda wako mwingi. Acha kung’ang’ania kufanya mambo yote wewe, wape na
wengine wakusaidie majukumu hayo ili kuokoa muda wako.
Kumbuka, muda ni kitu cha thamani sana ambapo ukijenga tabia ya kuutumia vizuri
utakuwezesha kufikia mafanikio makubwa yanajitokeza katika maisha yako.