Bw . Hassan Mtenga
Katibu wa Ccm Mkoa wa Iringa
CHAMA cha mapinduzi ( CCM) Mkoa wa Iringa kimelaani shambulio lililofanywa na wafuasi wa chama
cha Demokrasia na maendeleo ( CHADEMA) kwa wananchi waliokuwa wakitoka katika
mkutano wa kampeni za mgombea Urais wa CCM Dr John Magufuli juzi.
Katibu wa CCM mkoa wa Iringa Bw.Hassan Mtenga aliwaeleza
waandishi wa habari jana kuwa chama chake kinawapa pole wananchi waliopigwa na
wafuasi hao wa Chadema waliotumwa na Mgombea Ubunge wa Chadema jimbo la Iringa
Mjini Mchungaji Peter Msigwa.
Mtenga alisema kuwa idadi kubwa ya waliopigwa fimbo ni
wanawake kuwa tukio hilo
haliungwi mkono na udhalilishaji mkubwa kwa wanawake hao
Hata hivyo alisema kuwa vitendo hivyo vya Mchungaji Msigwa
kutumia vijana kupiga wananchi na wanachama wa CCM havivumiliki na kuwa iwapo
Mchungaji huyo akiendelea na vitendo hivyo na kukimbia Kama
ilivyokawaida yake sasa atambue wazi kuwa watamkamata na kumkapeleka polisi.
" Upole Wetu CCM ndio ambao umemfanya Mchungaji msigwa
kuendelea kuwafanyia vurugu wanachama wetu ila kwa sasa tutajitolea kumkamata
anaewatuma vijana hao kupiga wananchi"
Alisema hadi sasa zaidi ya wana CCM 7 katika jimbo la Iringa
Mjini wamevamiwa na kupigwa na wafuasi hao wa Chadema ambao wahifadhiwa katika
Gesti ya Sambala na nyingine hapa Mjini .
Akielezea kuhusu lugha za matusi anazozitoa Mchungaji Msigwa
kwa Mgombea Ubunge wa CCM jimbo la Iringa Mjini Bw Frederick Mwakalebela
alisema ni dalili za kuanguka kwa mchungaji Msigwa katika uchaguzi mkuu
Kwani alisema Kama angekuwa
ni mbunge aliyewatumikia vema wananchi kwa kutimiza ahadi zake asingekuwa
anatumia muda mwingi kutukana badala ya kueleza wananchi nini amefanya kwa
miaka mitano .
Hivyo alisema kuwa iwapo Mchungaji Msigwa angekuwa na uwezo
basi angesimama jukwaani kujibu zilipo Pesa za mfuko wa jimbo na kiasi cha tsh
milioni 340 alizopewa na Mgombea Urais wa Chadema Edward Lowasa .
Mtenga alisema ushindi wa Mwakalebela jimbo la Iringa Mjini
upo wazi kabisa na kuwa katika Mkoa wa Iringa kwa uchaguzi huu hakuna jimbo
litakalokwenda upinzani.