Mjumbe wa Kamati Kuu na Mwanasheria wa Chama cha Demokrasia
na Maendeleo (CHADEMA), Mabere Marando, amepelekwa nchini India na
familia yake kwa ajili ya kupata matibabu zaidi -- yameripoti magazeti la
MTANZANIA na MAJIRA siku ya Jumanne, Septemba 15, 2015.
Akizungumza na MTANZANIA Dar es Salaam jana, Ofisa Uhusiano
Msaidizi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), John Steven, alisema Marando
aliondoka juzi na baadhi ya ndugu zake.
“Wameondoka Jumapili
kwenda nchini India kwa ajili ya matibabu zaidi, wenyewe walisisitiza tusitaje
ugonjwa unaomsumbua ndugu yao, na kwamba ataeleza mwenyewe (Marando) pindi
atakapopona”
Marando ambaye pia ni Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CHADEMA,
alifikishwa hospitalini hapo usiku wa Septemba 7, mwaka huu, baada ya kuugua
ghafla akiwa nyumbani kwake na kuazwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete
karibu wiki nzima kwa ajili ya matibabu.