PICHA 12 ZA MAZISHI YA WAZIRI CELINA KOMBANI

MAKAMU wa Rais, Dk. Gharib Bilal na Waziri Mkuu, Mhe. Mizengo Pinda leo wameongoza mamia ya waombolezaji katika maziko ya aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Celina Kombani yaliyofanyika kwenye shamba lake lililopo Lukombe nje kidogo ya Mji wa Morogoro.

Kombani ambaye alikuwa mbunge wa Jimbo la Ulanga Mashariki alifariki dunia Alhamisi iliyopita katika Hospitali ya Andhraprasth Appollo ya mjini Delhi, India alikokuwa amelazwa akitibiwa saratani ya kongosho.

Viongozi wengine walioshiriki maziko ya Mhe. Kombani ni pamoja na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete, Spika wa Bunge Anne Makinda, Mgombea Mwenza wa urais kupitia CCM Samia Suluhu, IGP Mstaafu Omar Mahita na wengineo.

Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu Celina Kombani mahali pema peponi. AMEN.