Miaka miwili inayokuja itakuwa nyenye viwango vya juu zaidi
vya joto kote duniani kwa mujibu wa idara ya utabiri wa hali ya hewa nchini
Uingereza.
Ofisi hiyo inaonya kuwa kutashuhudiwa mabadiliko makubwa
huku gesi chafu zikitarajiwa kwa na athari katika mabadiliko ya hali ya hewa.
Kulingana utafti uliofanywa, unaonyesha kuwa msimu wa El
Nino kwa unashuhudiwa eneo la Pacific unatarajiwa kusambaa kote duniani.
Uchunguzi huo pia unaonyesha kuwa msimu wa joto barani ulaya
huenda ukawa wenye kibaridi kwa muda wakati sehemu zingine za dunia
zitakaposhuudia kupanda kwa viwango vya joto.
Mkurugenzi wa idara utabiri wa hali ya hewa nchini Uingereza
Prof Stephen Belcher, anasema , inaeleweka kuwa masuala ya asili huchangia
kubadilika kwa hali ya hewa kila mwaka lakini viwango vya juu vya joto vya
mwaka huu, ni ishata ya athari zinazochangiwa na kuongeza kwa gesi chafu
duniani.

