Kamanda wa Polisi
Mkoa wa Mbeya Ahmed Msangi.
Watu watano wamefariki dunia Mkoani Mbeya katika matukio matatu tofauti
likiwemo la ajali ya haice iliyosababisha vifo vya watu wanne mkoani hapa.
Katika tukio la kwanza gari
lenye namba za usajili T.519 Akh
aina ya Toyota Haice ikiendeshwa na dereva
asiyefahamika kugongana na pikipiki yenye namba za usajili T.535 Awc aina Ya T-Better eneo la Nanenane Jijini
Mbeya.
Ajali hiyo imetokea Septemba
29 majira ya Saa 4 usiku katika
eneo la Nane-Nane, Kata Ya
Isyesye, barabara Kuu ya Mbeya/Njombe .
Kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya Ndugu Ahmed Msangi amewataja
waliokufa katika ajali hiyo kuwa mwendesha
pikipiki ambaye bado jina lake halijafahamika sanjali na wengine watatu
raia wa Ethiopia ambao majina yao bado hayajafahamika mara moja ambao walikuwa wamepakizwa kwa pamoja kwenye pikipiki hiyo
kwa mtindo maarufu wa Mshikaki.
Aidha Katika ajali hiyo
Edward Aloyce (42) Mkazi Wa Uyole ambaye alikuwa abiria kwenye Haice alijeruhiwa na amelazwa katika Hospitali ya Rufaa Mbeya.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Ndugu
Msangi amesema chanzo cha ajali hiyo ni
mwendo kasi wa gari hiyo ya abiria pamoja na pikipiki hiyo.
Amesema dereva wa
hiace alikimbia mara baada ya kusababisha ajali hiyo ambapo jitihada za kumsaka
zikiendelea kufanyika na jeshi hilo
miili ya marehemu imehifadhiwa Hospitali Ya Rufaa Mbeya.
Katika tukio jingine mtu mmoja Mkazi wa
Masoko Wilaya ya Rungwe
Ndugu Tukupyelesya Enock
Mwakifuna (54) amefariki dunia mara baada ya gari walilokuwa wakisafiria T.913 Amb aina Ya Toyota Hillux ikiendeshwa
na dereva asiyefahamika kuacha njia na
kupinduka huko katika kijiji cha Masoko,
Wilaya Ya Rungwe, Mkoa Wa Mbeya bararabara ya Tukuyu/Lwangwa.
Aidha Katika ajali hiyo abiria Watatu wanawake wawili na Na
mwanaume mmoja walijeruhiwa na wamelazw katika hospital ya Hospitali ya Wilaya Rungwe huku chanzo cha .
ajali hiyo ni mwendo kasi dereva .
Kufuatia matukio
hayo Kamanda wa Polisi Mkoa Wa Mbeya Kamishna Msaidizi Mwandamizi Wa Polisi
Ahmed Msangi ametoa o wiito Kwa madereva
kuwa Makini wanapotumia vyombo vya moto
ikiwa ni pamoja na kuzingatia sheria na kanuni za usalama barabarani ili
kuepuka ajali zinazoweza Kuepukika.