THE game is over ! Sasa ni wazi kuwa familia ya staa
mkubwa wa muziki wa kizazi kipya Bongo, Nasibu Abdul ‘Diamond Plutnamz’
imemtema rasmi mzazi mwenzake Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ kwa kile
wanachodai …. “Tumechoshwa na uzungu wake”, Risasi Mchanganyiko linaweza
kuandika.
Chanzo kilicho karibu na familia hiyo kililiambia gazeti
hili kuwa kina taarifa kuwa mama Latiffa ‘Tiffah’ hatarejea tena nchini
kutokana na kushindwana na wanafamilia, kwani wanaendekeza uswahili, kitu
ambacho yeye hakiwezi.
“Familia ya Diamond ndiyo imemchoka, unajua yule hajazoea
mambo ya kiswahili swahili, ametofautiana nao sana na ndiyo maana hata wao
wamesema hawamtaki tena, wanahitaji mswahili mwenzao,” kilisema chanzo hicho.
FAMILIA YA DIAMOND
HII HAPA
Ili kujua ukweli wa maelezo hayo, mwandishi wetu
alimtafuta mama mzazi wa Diamond, Sanura Kassim ‘Sandra’ kupitia simu yake ya
mkononi, na alipoulizwa, alihamaki na kuanza kufoka, akidai hataki kuingiliwa
mambo yake ya ndani na kwamba kama kuna mtu anataka kujua zaidi amfuate Zari
huko kwao (South Afrika).
“Hata kama ni kweli, mimi na huyo sijui Zari wenu
tumegombana wewe yanakuhusu nini? sipendi kuingiliwa kwenye mambo ya familia
yangu, ninachojua ni kwamba hayupo hapa na maisha yanaendelea,” alisema Mama
Diamond na kukaa kimya huku simu ikiwa hewani.
Wakati simu ikiwa hewani, ghafla sauti ya kiume ilisikika
na kujitambulisha kwa jina la Anko Salum, aliyemtaka mwandishi kuachana na
habari hizo, kwani ni za ndani na zitamalizwa na wenyewe kama familia.
Wakati mwandishi wetu akiendelea kuzungumza na Anko
Salum, ghafla tena sauti nyembamba na kali masikioni ilisikika na mwanahabari
wetu akaibaini kuwa ni ya Esma, ambaye ni dada wa Diamond.
“Mbona mnatufuatilia sana jamani? Nani anafuatilia mambo
yenu? Nafasi ya Zari imefika mwisho, tunamkaribisha mwingine yeyote, kama kuna
msichana mrembo unamjua, tuletee nyumba yetu ni kubwa sana, na sisi
tunaruhusiwa kuoa hata wanawake wanne, Zari ameishia hapo, tena hatujagombana
naye, lakini tumechoshwa na uzungu wake, awamu hii tunahitaji mswahili
mwenzetu.
“Zari ameenda kwao, kulea watoto wake na kuangalia
ustaarabu mwingine, tunamtakia kila la kheri, lakini hatuna ugomvi naye
kabisa,” alisema Esma.Jitihada za kumpata Diamond hazikuzaa matunda kutokana na
namba yake ya mkononi kutokuwa hewani kila alipopigiwa, hata hivyo jitihada
zaidi zinaendelea kumtafuta.