Wakati Mbowe akisisitiza msimamo wa kuwataka wafuasi wa
Ukawa kutorudi nyumbani baada ya kupiga kura na badala yake kukaa umbali wa
mita 200 kutoka vituo vya kupigia kura ili kulinda kura zao, Jaji Mkuu Othman
Chande alikataa kuzungumzia suala hilo na badala yake kutaka mahakama iachiwe
ili itoe uamuzi wake kwa haki.
Jaji Chande aliyasema hayo jana wakati alipoulizwa na
waandishi baada ya kufungua mafunzo kwa majaji na Wasajili Mahakama Kuu Jijini
Dar es Salaam, juu ya wajibu wa mahakama katika uchaguzi mkuu na namna ya
kukabiliana na changamoto zilizopo katika kusimamia kesi za uchaguzi,
yaliyoandaliwa na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC).
Tayari Mahakama Kuu imeshapanga majaji watatu
kushughulikia suala hilo lililoibua mvutano mkali hivi karibuni baina ya
viongozi wa Ukawa na wakuu wa Nec na Jeshi la Polisi. Kesi hiyo itaanza
kunguruma rasmi leo.
Katika hatua nyingine, Jaji Chande alikiri kuwa uchaguzi
wa mwaka huu ni wenye mchuano mkali na kwamba mahakama zimejiandaa kumaliza
kesi zitakazotokana na uchaguzi huo kabla ya miezi sita inayotajwa kisheria.
Alisema mwaka 2010 kulikuwa na kesi 44 za uchaguzi kwa
ngazi za Ubunge na kati yake, 17 zilikwenda hadi hatua ya mwisho baada ya
kutolewa ushahidi huku nyingine zikiisha katika hatua za awali.
“Ushindani ni mkali katika uchaguzi huu, tunatarajia
kupokea kesi nyingi za uchaguzi. Tumejiandaa kupokea, kusikiliza kwa haraka ili
kuwezesha wapigakura kujua mshindi halali ni yupi,” alisema.
Akieleza zaidi, alisema sheria imeweka wazi kuwa
anayestahili kufungua kesi siyo mpigakura bali wagombea wenyewe.
Mratibu THRDC, Onesmo Olengurumwa, alisema wameshirikiana
na Ofisi ya Jaji Kiongozi kuandaa mafunzo hayo kwa kutambua kuwa ni wadau
muhimu katika kushughulikia kesi za uchaguzi ili kuwezesha haki kutendeka kwa
haraka
Goodluck Jonathan
Akiri Ushindani Ni
Mkali Kati Ya CCM
na UKAWA
Mkuu wa Jopo la Waangalizi kutoka Jumuiya ya Madola na
aliyekuwa Rais wa Nigeria, Goodluck Jonathan, amekiri kuwa uchaguzi wa mwaka
huu nchini Tanzania una ushindani mkali kutokana na namna vyama vilivyojiandaa
lakini akawataka wagombea wote wa nafasi za urais kujiandaa kukubali matokeo
kwa maslahi mapana ya taifa lao.
Wagombea wanaochuana kwa karibu ni, Dk. John Magufuli wa
Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Lowassa.
Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es
Salaam mara baada ya kuwasili nchini, Jonathan aliyekubali kuondoka madarakani
Mei mwaka huu na kumpisha Muhammad Buhari baada ya kushindwa katika uchaguzi
mkuu nchini mwake, alisema katika uchaguzi wowote kuna kushinda na kushindwa na
hivyo wagombea wajiandae kwa matokeo yoyote ili kuiacha nchi yao ikiwa salama.
Alisema ijapokuwa ushindani ni mkali, Jumuiya ya Madola
inaamini kuwa uchaguzi utakuwa huru na haki na kwamba imani yao kubwa ni
Tanzania kusimamia demokrasia iliyokuwapo wakati wote tangu ipatre uhuru wake
mwaka 1961.
Jonathan anaongeza jopo lenye waangalizi 14 kutoka
mataifa mbalimbali yaliyo wanachama wa Jumuiya ya Madola