Kumekuwa na ongezeko kubwa sana la magonjwa kama uzito
kupita kiasi,kisukari,cancer,uvimbe kwenye kizazi yote haya chanzo chake ni
kuongezeka kwa utaalamu katika vyakula vyetu vya asili ambavyo babu zetu
walitumia.
Leo ningependa kuongelea sana vyakula vifuatavyo ambavyo ni
vihatarishi vikubwa vya afya zetu.
1. Vyakula vya ngano
2. Vyakula vyenye sukari nyingi
3. Vyakula vyenye nyuzi nyuzi kidogo
UTANGULIZI
Tafiti zinaonesha kuwa vyakula tunavyo kula kama vyakula vya
ngano ambavyo vina kiambata mahususi kiitacho GLUTEN. Hii ni protini
ipatikanayo kwenye ngano ina gundi ambayo hushikilia chakula kwa pamoja. Pia
vyakula kama vyenye sukari nyingi na nyuzi nyuzi kidogo nazo ni chanzo kikubwa
cha matatizo sugu kama kisukari,uzito mkubwa na mengineyo.
SABABU
Utafiti unaonesha kuwa vyakula hivi huharibu ukuta wa
umeng'enyaji chakula kutokana na allergy ya hivyo vyakula. Kuta hizo za utumbo
mwembamba huvimba na kusababisha vyakula ambavyo avijameng'enywa vizuri kuingia
katika mzunguko wa damu na hatimaye kinga ya mwili huanza kupambana na hicho na
hatimaye kusababisha kusambaa kwa allergy mwili mzima na kuathiri utendaji kazi
wa insulini(insulin resistance). Insulin ni kichocheo kinachosawazisha sukari
mwilini.
Kuathiriwa kwa utendaji kazi wa hiki
kichocheo..kinarundikana mwilini na kusababisha matatizo makuu haya:
~Insulin huongeza uhifadhi wa mafuta mwilini na haya mafuta
huhifadhiwa kwenye sehem za kuhifadhi mafuta.
Ndio maana tafiti zinasema kuwa watu wengi wenye uzito
kupita kiasi ukiwapima utakuta kuna kiwango kingi cha insulin kwenye damu
lakini sukari ipo kawaida watu kama hawa tunawaita PRE-DIABETES. Asilimia kubwa
ya watu tupo katika hili kundi bali hatufanyi uvhunguzi. Hicho ni kiashiria
awali cha ugonjwa wa kisukari.
~Kiwango kingi cha insulin kinafanya mtu azeeke mapema hivyo
basi ni dhahiri kuwa watu wengi wenye kisukari hudhoofika na kuzeeka kwa kasi.
MIFANO YA TAFITI ZA KISAYANSI
~Utafiti uliofanyika dec,2007 ambao ulihusisha makundi makuu
mawili. Kundi la kwanza ni kundi la watu wenye uzito mkubwa kupita kiasi na
kundi la pili ni watu wenye uzito wa kawaida.
~~Utafiti huu ulizingatia kuangalia viashiria vya allergy
vitokanavyo na vyakula tunavyokula kama mikate na vyakula vyenye sukari
nyingi~~
1. C-reactive protein
~hiki ni kiashiria kuwa kuna mpambano unaendelea na
umesababisha allergy kwenye njia ya chakula
2. Kuziba kwa mishipa mikubwa ya damu eg Mshipa upelekao
damu kichwani CATOTID ARTERY kwa kutumia ultrosound
3. Kipimo cha damu kuangalia kiashiria cha allergy ambayo
huchelewa kujitokeza baada ya muda kidogo mwezi hadi week ukiwa umekula vyakula
hivi. Hiki kipimo kinaangalia kichocheo kiitwacho IgG.
MATOKEO
~Watu wenye uzito kupita kiasi walionesha kuwa na kiasi
kingi cha kiashiria namba moja C-reactive protein mara tatu ya watu wenye uzito
wa kawaida.
~Pia wenye uzito mkubwa walionesha kiwango kingi cha IgG
~Watu wenye uzito mkubwa walionesha kwa kutumia ultrasound
kuwa na mafuta mengi kwenye mishipa mikubwa ya moyo na inayopeleka damu
kichwani.
UTAFITI HUU LIFANYIKA KWA KUTUMIA VITU VIFUATAVYO
~Vyakula vya viwandani
~Antibiotics
~steroids
~Dawa za kuondoa allergy
~Vyakula vya sukari nyingi
~Vyakula vyenye fiber kidogo