KILIMO CHA MAPARACHICHI KIBIASHARA

Matunda ya Maparachichi yanazidi kuwa ni mazao ya muhimu katika nchi za joto na joto kiasi katika ulimwengu. Kutokana na taarifa ya mwaka 1976, nchi ya Mexico ndiyo inayozalisha kwa wingi duniani ikifuatiwa na Marekani na Brazil.

UZALISHAJI KATIKA AFRIKA.
Maparachichi, mara nyingi hupandwa mbegu zake, huzalishwa kwa ajili ya chakula cha nyumbani katika maeneo mengi Afrika. Hata hivyo ni nchi chache zimeweza kuendeleza uzalishaji kwa kiasi kikubwa kwa ajili ya uuzaji nchi za nje. Kwa sasa Maparachichi husafirishwa na kuuzwa ulaya kutoka Ivory Coast, Cameroon, Kenya, Swaziland na maeneo mengine ya kusini mwa Africa.

Maparachichi hustawi vizuri katika hali ya joto. Mimea ya Maparachichi hupandwa umbali wa mita 8 kwa mita 1. Katika eka moja kunaweza kukawa na idadi ya miti chini ya 400.

BIASHARA.
Kama kila mti utazaa matunda 50 kwa kiwango cha chini, kwa hiyo miti 400 itazaa matunda 400 * 50= 20,000. Ikiwa kila tunda litauzwa kwa shilingi 200 bei ya jumla, fedha itakayopatikana ni sh 20,000 *200 = 4,000,000/= zingatia kwamba hilo zao utavuna kwa muda mrefu sana.
Unaweza kununua miti ya Maparachichi iliyofanyiwa budding tayari na kupanda shambani kwako. Katika muda wa miaka mitatu utaanza kuvuna matunda.

Kwa nini Tanzania hatumo kwenye orodha ya nchi zinazozalisha Maparachichi wakati tuna eneo kubwa na hali ya hewa inayoruhusu karibu katika kila mkoa nchini kwetu? Ni jambo la aibu na fedheha kubwa kuona tuko nyuma kwa kila jambo. Wakulima sasa hebu tuamke na tuangalie fursa zingine ndani ya kilimo chetu.

Kuna mazao mengi sana ambayo kama mtu atajikita katika kuyafanyia kazi, mafanikio ya uhakika yatakuwepo. Kwa mfano kuna Miwa. Lima ekari moja ya miwa, ekari moja unaweza ukavuna miwa 100,000. Na kama utauza kila muwa kwa jumla Tshs. 300 utaweza kupata Tshs. 30,000,000/= hicho ni kiwango cha chini kabisa. Fikiria una ekari 10.

Kwa hiyo ndugu mkulima, hebu jaribu kuwaza zaidi ya hapo ulipo ili uweze kuona thamani ya kilimo. Tuondoe ile dhana ya kwamba kulima ni shida au mazoea.