MGOMBEA urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), John Magufuli
amemmwagia sifa lukuki, mkali wao ndani ya muziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul
‘Diamond’ kutokana na ushindi wa tuzo tatu za Afrimma zilizofanyika wikiendi
iliyopita nchini Marekani
Tukio hili lilitokea katika Viwanja vya Shule ya Msingi
Mpilipili mkoani Lindi baada ya staa wa Bongo Fleva, Ali Saleh Kiba kushuka
jukwaani kukamua kwenye kampeni za mgombea huyo wa urais, ndipo Magufuli
alishika kipaza sauti na kumsifia Diamond aliyeshinda tuzo za Msanii Bora wa
Kiume Afrika Mashariki, Msanii Bora wa Mwaka na Utumbuizaji Bora wa Video.
“Ukweli nampongeza sana
msanii Diamond kwa jinsi anavyojituma na kuipeperusha vyema bendera ya taifa
letu…,” alisema Magufuli huku pia akiwapongeza Ommy Dimpoz na Vanesa Mdee
walioshinda tuzo tofauti katika kinyang’anyiro hicho.
Aidha, katika kampeni hizo Magufuli aliwaahidi wakazi wa mji
huo kuwajengea Lindi mpya ambayo itakuwa ya neema kupitia gesi inayopatikana kwenye
ukanda huo, unafuu wa vifaa vya ujenzi ikiwemo saruji ‘cement’ iliyoanza
kupatikana kwa bei ya shilingi 8,000 kwenye kiwanda cha Dangote kilichopo
Mtwara, zao la korosho ambalo Magufuli alijinandi kuwa na digrii ya zao hilo .
