Rais wa Marekani, Barack Obama ametangaza kuwa vikosi vya
marekani vyenye silaha vimepelekwa Cameroon kusaidia mapambano dhidi
ya wanamgambo wa Boko Haram.
Kikosi cha wanajeshi 300, kitafanya operesheni za upelelezi,
kijasusi na operesheni za kipelelezi katika ukanda mzima.
Marekani imetambua ongezeko la tishio ambalo washirika wake
na nchi ambazo Marekani ina maslahi zinakabiliwa nalo kutoka kwa Boko haram
pamoja na kuwa majeshi ya Cameroon, Chad,Niger na Nigeria yamekuwa yakifanya
operesheni ya pamoja dhidi ya wanamgambo hao.
Mwaka jana ndege za upelelezi za Marekani na Wanajeshi
waliingia kaskazini mashariki mwa Nigeria baada ya kutekwa nyara kwa
zaidi ya wanafunzi wa kike 200 ambao bado hawajapatikana.
