Rapper aliyejiunga na kundi la ISIS, Deso Dogg auawa, aliwahi kufanya ziara na DMX

Mfuasi wa kundi la kigaidi la ISIS na rapper wa zamani, Deso Dogg ameuwa nchini Syria, Oct. 16 baada ya kushambuliwa na ndege za kivita za Marekani.

Deso Dogg ambaye alijulikana na pia kwa jina la Abu Talha al-Almani, aliwahi kufanya ziara DMX.

Rapper huyo alizaliwa nchini Ujerumani kwa jina la Denis Cuspert kabla ya kubadili jina na kuwa Abu Talha al-Almani. Aliacha kufanya muziki mwaka 2012 na kujiunga na ISIS.

Shirika la habari la AFP liliripoti November 2014 kuwa picha za Cuspert zilimuonesha akiwa ameshikwa kichwa cha mtu aliyeuawa kutokana na kuipinga ISIS.