Ronaldo ndani ya msimu wake bora zaidi na Madrid – hizi hapa rekodi zake

Katika msimu mpya wa soka barani ulaya Real Madrid wana rekodi ya kupiga mipira mingi zaidi langoni mwa wapinzani – mara 150 – na wamefunga magoli mengi (21) kuliko timu yoyote katika La Liga msimu huu.

Rekodi hii inamfanya Rafa Benitez atembee kifua mbele lakini inawezekana yote yasingewezekana bila Cristiano Ronaldo.

 Bila Ronaldo – Madrid ingepoteza asilimia 44 ya magoli (magoli 12) iliyofunga maimu huu katika mashindano yote (magoli 27). Mshambuliaji huyo Ureno hakuwahi kuwa wastani mzuri wa magoli yote ya Madrid kama alivyoanza msimu huu -: 37% in 2014-15 (magoli 61 kati ya 162), 32% msimu wa 2013-14 (51 kati ya 160), 36% msimu wa 2012-13 (magoli 55 kati ya 153), 34% msimu wa 2011-12 (magoli 60 kati ya 174), 36% msimu wa 2010-11 (magoli 53 kati ya148) na 27% msimu wa 2009-10 (magoli 33 kati ya 119).

Cristiano anaingia kwenye mchezo wa leo dhidi ya Las Palmas, wapinzani wake wa 58 tangu alipoanza kuichezea Madrid, CR7 leo atahitaji kuiboresha rekodi yake ya kufunga katika dimba la nyumbani kwenye ligi – ni goli moja tu kati ya 7 yaliyopita ndio amefunga Santiago Bernabeu.

RONALDO NDIO MCHEZAJI PEKEE AMBAYE HAYUPO KWENYE ‘ROTATION’ YA BENITEZ.

“Rotate Cristiano? Huyu ndio mchezaji anayefunga magoli mengi zaidi lazima acheze zaidi’ alisema Benitez mwezi mmoja uliopita. Ronaldo ndio mchezaji pekee ambaye amecheza kila dakika ya mchezo msimu huu. Hata Keylor Navas ambaye leo hatocheza hajacheza mechi zote msimu huu.