ALBUM YA ADELE YAVUNJA REKODI MAREKANI, YAUZA NAKALA MILLIONI 3.38 KATIKA WIKI YA KWANZA

Album mpya ya Adele, 25 imevunja rekodi kwa kuuza nakala milioni 3.38 katika wiki yake ya kwanza nchini Marekani pekee, kwa mujibu wa taarifa za Nielsen Music.

Staa huyo wa Uingereza amevunja rekodi hiyo tangu Nielsen ianze kufuatilia mauzo ya album mwaka 1991. 25 iliyotoka Novemba 20 imekuwa pia album ya kwanza kuuza nakala nyingi zaidi katika wiki ya kwanza.

Kwa Uingereza, 25 imevunja pia rekodi kwa kuuza nakala 800,000 katika wiki yake ya kwanza.