Haya ndio matumizi ya fedha ambazo ilikuwa zitumike sherehe za Uhuru December 9

Kwa sababu tayari Rais wa John Pombe Magufuli ametangaza kwamba sherehe za Uhuru siku ya December 09 2015 hazitokuwepo, ninayo taarifa nyingine kuhusu maamuzi mengine ya pesa ambazo zilitengwa kwa shughuli hiyo.

Taarifa kutoka Ikulu imetolewa kwamba fedha ambazo zilitengwa kwa ajili ya kutumika kugharamia sherehe za siku ya Uhuru ambazo zingefanyika December 09 2015, zitumike kufanya upanuzi wa barabara ya Mwenge hadi Morocco iliyopo Dar es salaam yenye urefu wa kilometa 4.3 kwa kuongeza njia za barabara za lami.

Taarifa hiyo ya Ikulu imesema tayari fedha hizo kiasi cha shilingi bilioni nne zimepelekwa kwa wakala wa barabara TANROADS kwa ajili ya utekelezaji wa agizo hilo.

Hii hapa taarifa yote ya Ikulu.