Kutekenya ni jambo lililowapa changamoto wanasayansi wengi wakiwamo Galileo, Francis Bacon na Plato. Waliumiza vichwa kujua kwa nini mtu hucheka au kushtuka anapotekenywa.
Wanasayansi wamekuwa wakijiuliza kwa nini watu hucheka wanapotekenywa ilhali tendo hilo ni la mguso?
Daktari katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa (Moi) iliyopo Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa John Kahamba anasema kitendo hicho hutokea baada ya ubongo kufanya kazi yake.
Anasema kwenye miili yetu kuna sehemu ya ubongo inayohusisha hisia kama kusikia, kuona, kupiga chafya au kuonja na vitu vyote hivyo hutafsiriwa kwenye ubongo.
“Kutekenya kunahusisha zaidi ngozi, ndiyo maana mtu akikugusa kidogo unapata hisia za kipekee ambao unaweza kukufanya ucheke au ukasirike,” anasema.
Anasema unapotekenywa taarifa hupelekwa kwa haraka hadi kwenye ubongo na kutuma ujumbe kisha ujumbe huo hutafsiriwa na kumpa binadamu taarifa. Hapo ndipo mtu huweza kucheka au kukasirishwa na kitendo hicho.
“Wapo wanaostahimili mtekenyo na wengine hawawezi kustahimili. Ndiyo maana wengine hawacheki wakitekenywa au wanatekenywa hawakasiriki, hawacheki lakini wanaruka na kujizuia au kukimbia,” anasema.
Kadhalika Profesa Kahamba anasema ubongo ni miongoni mwa maeneo magumu katika mwili kuyafafanua na kuelezea utendaji wake kwani hufanya kazi kwa kasi zaidi ya umeme.
Aina za mtekenyo
Wanasayansi wanazitaja aina mbili za mazingira ya kutekenywa. Kwanza ni gargalesis huku ni kutekenywa kwa nguvu kunakosababisha kicheko hasa pale unapotekenywa kwapani au tumboni.
Pili ni knismesis ambayo huhusisha mshiko mdogo wa kawaida kwenye maeneo yenye hisia na kusababisha mshtuko mdogo badala ya kicheko.
Kutekenya kunahusisha ubongo
Kitendo cha kutekenya na kucheka watafiti wanasema kinaandaliwa kwenye maeneo mawili ya ubongo ambayo yana wajibu wa kugundua mguso na hisia za raha au kero. Maeneo hayo ni somatosensori coteksi na anterior coteksi.
Utafiti wa wanasayansi wa Chuo Kikuu cha Tuebingen, wanasema mtu anapotekenywa hucheka kwa sababu ya kujilinda na si kuwa tendo hilo linachekesha.
“Maeneo yanayotekenywa ni maeneo yetu dhaifu ya mwili kama shingo, tumbo au kwapa, hivyo yanapoguswa mtu hucheka ili kuzuia kitendo kile,” wanasema watafiti hao.
Watafiti hao wanasema binadamu hujifunza kucheka pindi wanapotekenywa tangu wakiwa watoto wachanga na ili kujilinda na kuwa kicheko hicho ni kielelezo cha kujihami.
Kadhalika wanasayansi wamegundua kuwa baadhi ya watu hucheka hata kabla hawajatekenywa, kwa kutishiwa tu kuwa wanataka kutekenywa.
Mwanasayansi wa mishipa ya fahamu kutoka Chuo Kikuu cha Maryland, Baltimore, Robert Provine anasema kucheka baada ya kutekenya kunaunda upendo kati ya mzazi na mtoto.
“Kama mtu anasema anachukia kutekenywa hana sababu, kwani anasahau kuwa njia ya kwanza ya mawasiliano kati yake na mzazi ilianzia hapo,” anasema.
Kwa nini huwezi kujitekenya na kucheka?
Ingawa wanasayansi wanaeleza kuwa ukitekenywa unacheka, lakini ni vigumu kujitekenya wewe mwenyewe na kucheka.
Inaelezwa kuwa unapopanga kujitekenya, tayari ubongo wako huwa na taarifa hizo, hivyo unajiweka tayari kufahamu kuwa tendo gani linafuata jambo linalozuia kutekenyeka.
Kiuhalisia, tendo la kucheka au kupata hisia zozote baada ya kutekenywa hupungua kwa sababu sehemu ya ubongo inayosababisha kicheko baada ya kutekenywa huwa imepata taarifa.
Katika jarida la saikolojia na jenetikali lililoandikwa na Dk Clarence Leuba wa Chuo Kikuu cha Yellow Springs, Marekani, anaeleza kuwa watu hawawezi kujitekenya na kucheka kwa kwa kicheko cha namna hiyo kinahitaji mshtuko unaoundwa na watu wawili kama ilivyo kwa utani.
Daktari wa Saikolojia wa Chuo Kikuu cha Nairobi, Nuhu Odhiambo naye anasema kutekenya kunahusisha ubongo kwa kiasi kikubwa.
Lakini anasema jambo hilo ni la kisaikolojia pia kwani mtu akiwa na hasira hawezi kucheka hata akitekenywa.
“Kwa mfano mtu analia, halafu umtekenye unadhani atacheka? Kwa hiyo tendo la kutekenyeka na kucheka linahusisha hisia za mtu kwa wakati huo,” anasema.
Anaeleza zaidi kuwa mara nyingi marafiki, ndugu, wenza au watu wa karibu,ndiyo wanatekenyana na kucheka lakini si watu wasiofahamiana.
“Kwa mfano, umepanda daladala, akatokea mwanaume tu akakutekenya, unadhani utacheka lazima utashangaa kwanza na pengine kukerwa na kitendo chake,” anasema.
Dk Odhiambo anasema ubongo wa mtu ni eneo gumu na utendaji wake wa kazi ni mgumu kuufafanua, ndiyo maana baadhi ya matendo yanayofanywa na mwanadamu ni vigumu kueleza yanatokea vipi.
Mtaalamu huyu anaeleza zaidi kuwa maeneo yanayotekenyeka ni yale ambayo ni rahisi kujeruhiwa, hivyo ubongo hutoa tahadhari ya kujilinda.
“Ndiyo maana mtu hubana mikono au kuishusha shingo chini pindi anapotekenywa shingoni au kwapani, hapo ubongo umetoa tahadhari ya kujilinda,” anasema.
Mwanabaolojia Charles Darwin na mwanasaikolojia Ewald Hecker, wanasema kucheka na kutekenywa vina uhusiano kwa kuwa vyote vinahusisha hisia za furaha. Wanasema mtu hawezi kucheka mpaka awe na hisia za furaha au atekenywe na mtu anayemfahamu.
Pia, Darwin katika utafiti wake anasema watu hutofautiana maeneo ya kutekenywa. Kwa mfano, wengine watacheka wakitekenywa miguuni, wengine shingoni au tumboni.
Baadhi husisimka wanapotekenywa maeneo ya miguuni, lakini hucheka wakitekenywa kwapani.