Mfuko wa kumsaidia mke, mtoto wa Mawazo kuanzishwa

Mwili wa aliyekuwa, Mwenyekiti wa Chadema mkoani Geita, Alphonce Mawazo (Savimbi) umezikwa leo saa tisa alasiri kijijini kwao Chikobe Jimbo la Busanda mkoani Geita nyumbani kwa mjomba wake, huku simanzi, vilio na majonzi vikitawala.

Katika mazishi hayo, Mwenyekiti wa Chadema taifa, Freeman Mbowe alisema, ilikumuenzi Mawazo Chadema wataanzisha mfuko maalum utakao julikana kwa jina la Alphonce Mawazo Trust Fund, ili kumsadia Mtoto wa marehemu, Precious na Mama wa marehemu Hellena Gidioni,

Pia, Mbowe alisema,fedha zilizochangwa na wabunge wa Ukawa Sh33.9 milioni zitawekwa kwenye mfuko huo na michango mingine, huku akiahidi kuhuisimamia mfuko huo, ili usije kuleta mfarakano na utumike vizuri ilikumuenzi Mawazo.

Mazishi hayo yaliongozwa na  Mwenyekiti huyo wa Chadema  Mbowe,  Mawaziri Wakuu wa wastaafu, Edward Lowassa na Federick Sumaye, wabunge wa Ukawa na viongozi waandamizi wa chama hicho.

Mwili wa Mawazo ulitolewa nyumbani kwao saa 5:51 asubuhi, na kupelekwa kwenye uwanja Chikobe uliyopo mitata chache kutoka nyumbani kwao, huku mvua kubwa ikinyesha.

Aidha Mwili wa Mawazo ulibebwa na walinzi wa Chama hicho (Red Brigade) kutoka nyumani kwao hadi kwenye viwanja hivyo ambapo ibada ya kumuombea ilifanyika kuanzia saa 6:40 mchana.

Wakati wa utoaji wa heshima za mwisho kwa mwili wa mwanasiasa huyo, idadi kubwa ya watu hasa akinamama na vijana walionekana wakipoteza fahamu, huku wengine wakilia kwa sauti kubwa.

Kabla ya mwili wa Mawazo kuzikwa wakazi wa kijiji cha Chikobe walipata nafasi za kutoa heshima za mwisho kwenye viwanja hivyo akiwemo mama yake mzazi Hellena Gidion na wanafamilia.

Viongozi wa Chadema waliwasili Kijijini hapo 6:35 wakitokea mkoani Mwanza, ambapo mara baada ya kuwasili ibada ya kumuombea marehemu ilifanyika.

Jana kijijini hapo askari polisi walionekana wakimalisha ulinzi wakati shughuli za mazishi ya Mawazo zikifanyika.

Wakati wa shughuli za kuaga mwili huo nyimbo mbalimbali zilizotungwa maalum kwa Mawazo ziliimbwa, huku baadhi ya jumbe zake zikipigwa na kuamsha hisia za wutu.

Baadhi ya jumbe zake ni pamoja na , “Nitakufa kwa kupigania haki za watoto wa taifa hili.”

Mbowe atoa shukrani
Akitoa salamu za pole, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alisema anawapongeza familia kwa kuwa na uvumilivu ili haki itamalaki.

Alisema watawala ambao wanajua nani alimuua Mawazo walijitahidi ili wasimuage, kwa sababu wanajua umuhimu wa Mawazo na kwamba walijitahidi kuzuia haki yake ya Kikatiba asiagwe, lakini ilishindikana.

“Mawazo alitoa maisha yake kupigania haki, ndugu zangu wa Chikobe, Busanda mlikuwa na hazina kubwa, mmewaona viongozi wengi waliyokuja hapa, sio kwamba Mawazo alikuwa tajiri sana, msomi, lakini alikuwa mstari wa mbele kutafuta ukombozi kwa kupigania haki za wanyonge,”alisema Mbowe.

Mbowe alisema wao kama Chadema wataendelea kupigana ilikuhakikisha watu wote waliyomuua Mawazo wanajua thamani ya Mawazo, na wanakamke na kwamba lazima wachukukuliwe hatua, kwani wanajulikana.

“Leo sitaki kuzungumza sana, lakini nataka niseme lazima sisi kama chama cha demokrasia tuhakikishe wale waliyohusika wanapatikana,”alisema Mbowe.

Mbowe alisema Mawazo alikuwa mstari wa mbele kudai haki na mkweli na kwamba  hakuwa muongo, alikuwa mkweli ndio mana hakujenga  Hekaru kijijini kwao.

“Chadema tutaanzisha  mfuko maalum utakao julikana kwa jina la Alphonce Mawazo Trust Fund, na fedha zilizochangwa na wabunge Sh33.9 milioni zitaingizwa kwenye mfuko huo na kwamba  utakuwa wa mtoto wa Mawazo na Mama wa marehemu, ilikutambua mchango wa Mawazo na kumuenzi,”alisema Mbowe.

Lowassa hautubia kwenye mvua
Akitoa salamu fupi jukwaani, huku mvua ikinyesha, Lowassa aliyekuwa mgombea urais katika uchaguzi mkuu uliopita kupitia Chadema,alitoa pole kwa mama mzazi wa marehemu, huku akimtaka awe jasiri katika kipindi hiki kigumu.

“Nimezungumza mengi jana na juzi, lakini mimi nataka nimpe pole mama wa marehemu, na mungu atazidi kukutia nguvu, sisi tupo na nyie pamoja na kamwe hatuwezi kuwaacha,”alisema Lowasa’

Lema
Akitoa salamu za rambirambi rafiki wa marehemu, aliyekuwa mbunge wa Arusha mjini, Goldbres Lema alisema,yeye ndiye alimuingiza Mawazo kwenye masuala ya siasa  na kwamba atakuwa begakwabega na familia ya marehemu katika kipindi chote cha maisha yake.

“Mimi nasimama hapa kama rafiki wa  marehemu,mimi ndiye niliyemuingiza kwenye siasa,Nampa pole mama mzazi, kwani Mama mwanao amekufa kishujaa, alikuwa mtu mwema, kilichomuua ni kupigania haki za nchi,alisema na Kuongeza Leman a kuongeza:

“Kazi njema aliyoifanya Mawazo haitasahaulika na kwamba naomba familia ya marehemu hasa mtoto wake, nimwambie sisi baba zake tupo tutamuangalia kwa kila jambo katika maisha yake,”

Aidha, Lema ambaye ni mgombea Ubunge jimbo la Arusha mjini kwa sasa, alisema Marehemu kafa kifo cha kinyama, na kwamba Chadema kinaamini huko alipo atakuwa yupo nyumbani kwa baba Mungu. “Wito wetu waliyotekeleza mauaji hayo wakamatwe mara moja, wanajulikana na tunawajua.”

Katika hali ya kushangaza walinzi Chadema waliwakamata watu na kwa sababu ambazo azikujulina ana kuwahoji katika viwanja vya kutolea heshima za mwisho kijijini hapo.

Mwili wa Mawazo ulizikwa kwa heshima zote jana.

Historia ya Marehemu.
Historia ya marehemu ilitolewa katika viwanja hivyo ilionyesha kwamba, Mawazo alizaliwa Disemba 28,mwaka 1976 katika kijiji cha Isungag’holo  Wilaya ya Sengerema Mkoa wa Mwanza, mwaka 1987-1993 alijiunga na elimu ya Msingi katika shule ya Chemamba na baadaye mwaka 1994-1997 alijiunga na elimu ya Sekondari Geita na 1998-1999 alijiunga na kidato cha tano na sita katika shule ya Seminari Luzangi Tabora.

Historia hiyo iliyosomwa na Semen Paulo kwa niaba ya Familia ilisema kuwa,Mawazo alijunga na Chuo cha Ualimu Butimba na kupata stashahada ya ualimu na kusoma digri ya biashara na Utawala.

Alijiunga na siasa mwaka 2010 kupitia chama cha TLP akiwa diwani wa Kata ya Sombetine mkoani Arusha, baadaye alijiunga Chama cha CCM Mwaka 2011 kabla ya kuhamia Chadema kuendelea na nafasi hiyo mkoani Mwanza na Geita.

Mawazo,alifariki dunia Novemba 14,wakati madaktari wa Hospitali ya wilaya ya Geita wakijaribu kuokoa maisha yake bila mafanikio kufuatia kushambuliwa na kundi la watu waliokuwa na silaha za jadi wanaosadikiwa kuwa ni wafuasi wa CCM.

Mwili wa Mawazo ulizikwa, huku mvua kubwa ikinyesha.

Wakazi wa Chikobe wamzungumzia
Wakimzungumzia Mawazo wakazi wa Kijiji cha Chikobe ambapo ndio nyumbani kwao walisema,tukio la kifo cha Kiongozi huyo ni la kusikitisha huku wakiitaka serikali kuhakikisha inachukua hatua kali.

Semen Paulo,alisema “Tukio la kifo cha Mawazo,lilinishutua sana,wakati linatokea nilikuwa safari..kwa kweli liliniskitisha na kama tumefikia hatua hii katika siasa tunaelekea kubaya”.

Akamatwa Akimpiga Picha Lowassa.
Mtu mmoja ambaye hakufahamika jina lake alikamatwa na walinzi wa Chadema wakati shughuli za kuaga mwili wa Marehemu zikiendelea.

Mtu huyo ambaye alionekana kijana akiwa amevalia sare za Chadema,alikamatwa wakati akimpiga picha Lowassa kwa kile kilichodaiwa kwamba alikuwa mfuasi wa CCM.